Na Mwandishi Wetu, Dodoma


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza hospitali ya CCBRT kwa kusaidia watu mbalimbali wenye uhitaji na kuahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuboresha afya na maisha ya Watanzania wote.

Akizungumza alipotembelea banda la CCBRT wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma jana, Waziri Mkuu Majaliwa mbali ya kuipongeza hospitali hiyo alisema serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Raisi Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

“Tunawapongeza sana CCBRT katika kuwasaidia watanzania wenye uhitaji. Sisi serikali peke yetu hatutaweza hivyo ushirikiano wa wadau yakiwamo mashirika yasiyo ya kiserikali ni muhimu sana na tunawahakikishia ushirikiano zaidi,” amesema mheshimiwa Majaliwa.

CCBRT ilitoa jumla ya baiskeli za walemavu maarufu kama viti wwendo tisa kwa ajili ya walemavu mbalimbali wenye uhitaji huku ikiahidi kuendelea kurejesha zaidi kwa jamii na watu wenye uhitaji.

Mheshimiwa Majaliwa alisema CCBRT imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua na kuleta maendelea katika sekta ya afya hapa Tanzania.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT, Bi Brenda Msangi alisema CCBRT na washirika wake wataendelea kuboresha mfumo wa huduma ya afya hapa nchini na kutoa kipaumbele kwa watu wenye uhitaji.

“Mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali kwetu CCBRT ni muhimu sana kuuonyesha umma wa Tanzania huduma mbali za kitaalamu zinazopatika katika Hospitali ya CCBRT,” alisema Bi Msangi.

Mmoja wa wanufaika wa viti mwendo Chipegwa Zayeye aliishukuru Hospitali ya CCBRT kwa msaada aliopewa kwani utasaidia maisha yake kuwa mepesi na kufanikisha ndoto zake katika maisha.

“Nimefurahi sana kupata hiki kiti mwendo. Asante sana uongozi na timu nzima ya Hospitali ya CCBRT kwa kuwajali watu wenye ulemavu na uhitaji pia,” alisema Chipegwa na kuongeza kuwa taasisi zingine ziige mfano huo.

pamoja na kuendelea kutibu ulemavu kama vile mguu kifundo, mdomo wazi, fistula na mtindio wa ubongo, Hospitali ya CCBRTinatoa huduma zote za afya za kibingwa na kibobezi zikiwemo kusafisha figo(dialysis),meno, maskio,pua na koo,macho na miwani,vipimo, maabara, matibabu ya wajawazito,magonjwa ya akana mama na mfumo wa uzazi, mifupa,kliniki za watoto, magonjwa ya ndani, fiziotherapia na magonjwa ya ngozi.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi Chipegwa Zayeye ambaye amepewa kiti mwendo na Hospitali ya CCBRT alipotembelea banda la CCBRT wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma jana. Wengine wa pili kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima na  na Mkurugezi Mtendaji wa CCBRT, Bi Brenda Msangi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...