Mkuu wa wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe (aliyesimama), akihutubia katika hafla ya kupokea vitabu vya masomo ya sayansi nakala 786 kwa kidato cha tano na sita na kemikali za maabara kwa ajili ya masomo kwa vitendo. Mchango huo umetolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), kama juhudi za kuiunga mkono Serikali katika kuhamasisha wanafunzi kusoma na kupenda masomo ya sayansi. Katika picha, wa pili kutoka kulia ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Evaclotida Kapinga (kulia) na Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Arusha, Christopher Anyango (kushoto). Hafla hiyo imefanyika katika Shule ya Sekondari Mkata, Oktoba 18, 2022.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika hafla ya kikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi na kemikali za maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi kwa vitendo kwa wanafunzi wa shule za sekondari za wilaya ya Handeni. Vitabuna kemikali hizo zimekabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya ya Handeni.
Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (GCLA), Evaclotida Kapinga (aliyesimama), akiwasisitizia jambo wanafunzi kuhusu umuhimu wa kusoma na kupenda masomo ya sayansi pamoja na kuwahimiza walimu kuendelea kutoa mchango wa elimu bora katika masomo ya sayansi.
Picha ya juu: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkata wakisikiliza hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali wakati wa hafla ya kupokea vitabu vya masomo ya sayansi nakala 786 na kemikali za maabara kwa ajili ya masomo kwa vitendo.
Picha ya chini: Baadhi ya wazazi na walimu wakiwa katika hafla.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati), akionesha aina ya vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, ambavyo ni vya masomo ya Baiolojia, Kemia, Hisabati na Fizikia kwa kidato cha tano na sita. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchembe na kulia ni Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Christopher Anyango.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...