Na Mwamvua Mwinyi,Pwani


MKURUGENZI wa mradi wa uzalishaji mchele na mashamba ya mpunga (MBAKIAMTURI )Kibiti Mkoani Pwani,Khamis Kambanga ametoa kilio chao kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuwasaidia banio lenye gharama ya sh.bilion tatu, ili kuongeza uzalishaji mpunga mara mbili kwa mwaka pamoja na kuwa na uhakika wa chakula.

Aidha amemuomba kwenda MBAKIAMTURI kujionea uzalishaji wa mpunga wa kiangazi na juhudi wanazozifanya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuinua sekta ya kilimo nchini.

Ametoa kilio hicho ,katika banda la kilimo Kibiti wakiwemo MBAKIAMTURI ,wakati Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas alipotembelea banda hilo katika maonyesho ya tatu ya wiki ya biashara na uwekezaji Mkoani Pwani yanayofanyika Mailmoja Kibaha Mjini.

Kambanga alieleza, nia yao kubwa ni kuongeza uzalishaji wa mpunga mara mbili kwa mwaka lakini wanakwama kwa kukosa banio .

"Matunda haya ni matunda yako wakati ulipokuwa mkuu wa wilaya ya Kibiti, Leo hii tunalima mpunga wa kiangazi kwa kutumia diezel ,unakuta mashine inaharibika ,mpunga unakauka , Waziri angetusaidia kutuunganisha na mdau , Taasisi kutujengea banio basi kero hii itakwisha"

"Kupatikana kwa banio itaondoa baa la njaa katika Taifa ,tutakuwa na uhakika wa Chakula kwa afya ya watu,"alifafanua Kambanga.

Kambanga alimsihi Bashe pia aende kutembelea umoja huo Kibiti ili kuona namna juhudi zao katika kuzalisha mpunga na bidhaa ya mchele.

Changamoto nyingine alitaja ni ukosefu wa mawasiliano kutofika MBAKIAMTURI ,kero hiyo inawasababishia kutumia sh.50,000 kwa kupanda bodaboda kwenda Ikwiriri kufuata mahitaji ambayo ni madogo kwa nauli wanayotumia.


Hata hivyo,alieleza kuwa wamelima kwa majaribio mpunga wa kiangazi hekari 380 na wanatarajia kuvuna mwezi Disemba mwaka huu.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Ahmed Abbas aliwapongeza MBAKIAMTURI kwa kufanya mradi huo,na kikubwa ni kupata ushirikiano ili waweze kuzalisha zaidi.

Alisema ,kilio Cha ukosefu wa mawasiliano ,ataangalia namna ya kufikisha changamoto hiyo kwa Waziri mwenye dhamana ili kutatua changamoto hiyo ,ikiwa ni moja ya kuweka Mazingira Bora ya uwekezaji huo wa mpunga.

Alisema ,Mtwara wanajivuna Kuwa na visima vya gesi na pia kunaanzishwa mradi mwingine wa gesi Huko Lindi .

"Vilevile tunakivutio Cha mnyama Nyangumi ,ambae anapiga Julai-Disemba kutoka Kusini kwenda Kaskazini kujizalia na kisha narudi kulea watoto wake,"Mnyama huyu hapatikani sehemu yeyote na huwezi kumuona kwa uwazi"

Abbas alisema,mnyama huyo akifika soko la Mnazibei anatoka nje kusalimia wananchi kwa masaa matatu kwani ni njia wanayopita kwenda kuzaliana Maeneo ya Kusini .

Alitaja fursa nyingine ya uhitaji wa Chakula Comorro , hivyo wafanyabiashara wanaweza kusafirisha chakula kwenda Comorro kwa njia ya Usafiri wa maji kwa masaa 8 na kwa usafiri wa anga ni dakika 45 hadi lisaa limoja.

Kwa upande wake, Ofisa kilimo ,mifugo na Uvuvi Kibiti, Bwenda Bainga alieleza eneo la MBAKIAMTURI lina ukubwa wa hekari 15,550 kwa uwekezaji wa kuzalisha mchele na kilimo Cha mpunga .


"Lengo lao wanataka kuongeza magunia kwa hekari kwani kwa Sasa wanapata gunia 15 kwa hekari mahitaji ni kupata gunia 40 kwa hekari hatua ambayo itasaidia kuongeza mapato ya halmashauri kwa ushuru utakaopatikana kwenye mchele ,ambapo kwasasa mchele mapato ambayo kwasasa ushuru unaotokana na mchele ni sh. milioni 250lengo kukusanya milioni 500":"alisema Bainga.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...