Mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya uwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Babati vijijini Ezekiel Dangalo ameamua kujitoa katika uchaguzi kwa madai ya kuwa na hofu ya kushindwa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa awali.

“Nimeamua kujiondoa baada ya kuona vichwa ni vilevile vilivyonipiga vibaya kwenye uchaguzi wa awali hivyo nimeogopa” amesema mgombea huyo.

Hata hivyo kwa mujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi, mgombea haruhusiwi kujiondoa siku ya uchaguzi, hivyo wajumbe wanaweza wakaamua kumchagua ama wasimchague.

Leo oktoba 2,2022 chama cha mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti wake wa taifa Samia Suluhu Hassan, kinafanya uchaguzi kuchagua viongozi katika ngazi za wilaya ambao wataongoza kwa kipindi cha miaka mitano.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...