Taasisi ya Benjamini William Mkapa Foundation imeshauri uwepo wa Kamisheni Huru ya kupitia gharama za huduma za Afya ikiwa ni pamoja na gharama za dawa, vifaa tiba, vitendanishi, na gharama za uendeshaji wa huduma, kama mishahara ya watumishi na tozo mbali mbali zilizo katika sekta ya Afya hapa nchini.
Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Programu za Uboreshaji wa Huduma za Afya wa Taasisi hiyo, Hendry Samky (pichani juu) walipokaribishwa wadau kutoa maoni yao kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu uboreshaji wa muswada wa Bima ya Afya kwa Wote kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, Dodoma Oktoba 19, 2022.


Samky akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Dkt. Ellen Mkondya -Senkoro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo akiongoza mkutano huo wa wadau.

Baadhi ya viongozi wa dini wakishiriki katika mkutano huo

Baadhi ya wadau waliohudhuria kutoa maoni yao kuhusu muswada wa Bima ya Afya kwa Wote.



Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.







 

Afisa Habari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Grace Kisinga (kusto) akiwa na Afisa Habari wa Wizara ya Afya, Catherine Sungura wakifuatilia kwa makini maoni ya wadau.

 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...