SHIRIKA Shirika la Tanzania Health Summit (THS) limeandaa mkutano mkuu wa 9 wa wadau wa sekta ya afya utakaoanza tarehe 11 hadi 13 Oktoba 2022, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Philip Mpango ndiye atakayeongoza mkutano huo, utakaoshirikisha watoa mada zaidi ya 40 kutoka nchi kadhaa barani Afrika na kwingineko.

Chini ya kaulimbiu “Ubora wa Huduma ya Afya Tanzania: Hali ya Sasa na Maboresho yanayohitajika ili kutekeleza Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya wa Tano (HSSP V)”, wadau katika mkutano huo watajadili hali ya sasa na maeneo ambayo yatahitaji rasilimali na jitihada zaidi ili kutimiza malengo.

Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya, unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi na kutekelezwa na Taasisi ya Uswisi ya Tropical and Public Health Institute ni miongoni mwa wafadhili wakuu wa mkutano huo. HPSS inalenga katika kuendeleza juhudi za ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora za afya kwa Watanzania.

"Wakati wa mkutano huo, mradi wa HPSS Tuimarishe Afya utaelezea mchango wake katika kufanikisha Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya wa Tano (HSSP V) kupitia ubunifu wa mradi, hususan Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) na mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa bidhaa za afya (Jazia Prime Vendor System)", alisema Ally Kebby, Meneja wa Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya.

Zaidi ya hayo, mradi wa HPSS utawasilisha matokeo yake mbalimbali ya utafiti ambayo yanatoa ufahamu katika mbinu zake zakusaidia utekelezaji wa HSSP V katika kongamano litakalofanyika Jumatano, tarehe 12 Oktoba 2022 yenye kauli mbiu: “Kutekeleza Mpango Mkakati wa Sekta ya AfyaTanzania.

Uliopita na michango ya sasa ya Mradi wa ushirikiano kati ya Serikali za Uswisi na  Tanzania wa HPSS Tuimarishe Afya” Pia, mkutano huo utatoa zaidi ya mawasilisho 100 ya matokeo ya tafiti za mashirika mbalimbali kuhusu afua mbalimbali za afya. Maazimio ya mkutano huo yataingia katika agenda ya Mkutano wa 23 wa Pamoja wa Mapitio ya Kiufundi ya Sekta ya Afya utakaofanyika mwezi Novemba 2022 na Mkutano wa Mwaka wa Mapitio ya Sera ya Sekta ya Afya utakaofanyika mwezi Desemba 2022 .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...