Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai amesema kuwa mpango wa kusambaza dawa kwa kutumia ndege isiyo na rubani aina ya Drone si kipaumbele chao kikubwa, bali kipaumbele ni kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wingi nchini.
Tukai amebainisha hilo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari -MAELEZO jijini Dodoma Oktoba 17, 2022, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya bohari hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Gerson Msigwa akihitimisha mkutano huo kwa kutoa pongezi kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD,Tukai kwa kueleza na kufafanua vizuri majukumu ya bohari hiyo.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Tukai pamoja na mambo mengine akielezea kuhusu mpango huo wa Drone kupata kifafa.... IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...