Baadhi ya wanachama wa CCM Wilaya ya Kibiti wakiwa katika zoezi la kupiga kura
Mwenyekiti mteule  wa CCM Wilaya ya Kibiti aliyechaguliwa janaOktoba 2 
Juma  Kassim Nderuke  aliyekaa katikati akiwa anasubiri kwenda kupiga kura akiwa amekaa na baadhi ya wajumbe  ndani ya ukumbi wa uchaguzi.

Na Khadija Kalili, KIBITI
KIJANA Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibiti alipindua meza kwa kupata ushindi wa kishindo kwa kutwaa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani Juma Kassim Ndaruke ambaye ameibuka kidedea kwa kupata kura 428 huku Mwenyekiti aliyekua aliyemaliza muda wake Abdullatif Jabir Malombwa aliyepata kura 385.

Uchaguzi huo ambao ulionekana kuwa na ushindani wa hali ya juu huku uongozi uliomaliza muda wake ukionekana kuwa na wafuasi kadhalika kwa yoande wa kundi la vijana wakionyesha kuwa na kiu ya kunyakua taji hilo ikiwa ni katika lengo lakundeleza gurudumu la maendeleo Wilayani Kibiti.

Awali ya yote uchaguzi huo ulianza ukiwa katika ulinzi wa hali ya juu ambapo vyombo vya usalama wakionekana kuimarisha ulinzi pamoja na TAKUKURU wakiwepo eneo.la tukio na kuonekana kusimama imara.

Aidha uchaguzi huo ulisimamiwa na Katibu wa Jumuia ya Wanawake Mkoa wa Pwani Fatma Juma Ndee ambapo kabla ya kuanza kwa uchaguzi alitangaza zoezi la kuwahakiki wajumbe wote kutoka katika kata 16 za Kibiti ambapo pia waliweza kuwabaini baadhi ya wapigakura ambao waliku wajumbe feki na kuamuru vyombo vya usalama kuwatoa nje na baada ya hapo zoezi liliendelea.

Wengine walioshiriki kwenye kinyang'anyiro hicho ni Mwenyekiti aliyekua aliyemaliza muda wake Abdullatif Jabir Malombwa aliyepata kura 385 huku akifuatiwa na Abdallah Seif Mpili aliyeambulia kura 7.

Aidha Wajumbe waliochaguliwa katika mkutano huo wajumbe wa mkutano mkuu Taifa CCM ni Ally Seif Ungando ,Khalid Mtarazaki na Rehema Jumanne Mkumba.

Wajumbe wengine wa mkutano mkuu CCM Mkoa ni Ashura Matimbwa na Uwesu Mtandika.

Baada matokeo kutangazwa Halmashauri Kuu CCM Wilaya ilikaa kikao na kumchagua Katibu Mwenezi wa Siasa na Itikadi ambaye aliyeshinda ni Juakali kuwa ndiye Katibu Mwenezi CCM Wilaya ya Kibiti.

Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mheshimiwa Twaha Mpembenwe alisema amesuuhudia uchaguzi huo kuwa ulikuwa wa haki na umezingatia kanuni na katiba ya Chama cha Mapinduzi hata kuweza kuwapata viongozi waliopata nafasi walizoomba akiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo.

Alisema hanashaka na maamuzi ya WANACCM waliyofanya kumchagua Mwenyekiti wa CCM waliomchagua hasa kwa uzoefu aliokuwanao wa kuongoza jumuhiya ya Vijana wa CCM katika miaka mitano iliyopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...