MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoani Tanga Audrey Claudius akizungumza wakati wa wiki ya huduma kwa wateja


MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoani Tanga Audrey Claudius akizungumza wakati wa wiki ya huduma kwa wateja


MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Mkoani Tanga Audrey Claudius akionyesha




,Afisa Mkuu NSSF Mkoa wa Tanga,Abubakari Mshangama kushoto akimuelekeza jambo mmoja wa wanachama wa mfuko huo

,Afisa Mkuu NSSF Mkoa wa Tanga,Abubakari Mshangama kushoto akimuelekeza jambo mmoja wa wanachama wa mfuko huo


Na Oscar Assenga,TANGA


MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF) wameadhimisha siku ya wateja duniani huku wakiwataka waajiri mkoani Tanga kuhakikisha wakati wanalipa michango yao kwa kutumia mifumo ya kieletroniki ili kurahirisha mwanachama aweze kulipwa papo kwa papo.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko huo mkoani Tanga Audrey Claudius wakati akizungumza kwenye wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika kwenye ofisi zao Jijijni Tanga

Meneja huyo alisema lazima taarifa za mwanachama ziwe kamilifu ndio maana wanasisitiza waajiri kuanzia sasa kutumia mfumo huo ambao utawezesha mnufaika kuweka kulipwa kwa wakati.


Alisema katika wiki hii watahakikisha wanachama wote wanaowadai watawalipwa ndani ya siku moja huku aliwataka waajiri wawawasaidie kulipa michango kwa kufuata mifumo na walipe kila mwezi.

"Lakini pia niwatake waajiri kuacha kulimbukiza michango kwani kufanya hivyo kunasababisha usumbufu kwa wanachama wanapo kwenda kufungua madai hivyo tuhakikishe tunalipa kwa wakati"Alisema Meneja huyo

Hata hivyo aliwataka waajiri mkoa wa Tanga kuhakikisha wanalipa michango yao na wenye malimbikizo wamepewa mikataba ya namna ya kulipa michango huku akiwasisitizia walipe kufuatana na mikataba waliopewa.

Awali akizungumza ,Afisa Mkuu NSSF Mkoa wa Tanga,Abubakari Mshangama alisema katika wiki ya huduma kwa wateja wameweza kutoa huduma mbalimbali ikiwemo ya huduma ya mtandao ambao utawawezesha wanachama hao kuweza kupata taarifa zao.

Mshangama alisema kwa waajiri wanaweza kutumia member portal hiyo wanaweza kuwasiji wanachama na kulipa michango yao ikiwemo kupata taarifa mbalimbali za Shirika hilo.

Aidha alisema wiki hii wanatoa elimu zaidi kuhusu huduma hizo za kimtandao huku akiwataka wananchi kujiunga na Shirika hilo ili kuweza kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa

Naye kwa upande wake mwanachama wa Mfuko huo Modo Mkufya alisema Mfuko huo wanaiomba Serikali waboreshewe pensheni hizo kidogo.

Awali naye Catharine Ramadhani alisema wamefurahi kushiriki kwenye wiki hiyo huku nakiomba huduma ziboreshwe ikwemo kuhakikisha wanaondoa vikwazo ambavyo vimekuwa vikijitokeza awali.

Alisema kwamba huduma za Mfuko huo ni nzuri huku akiwataka wananchi wengine wajiunga nao ili kuweza kunufaika na mafao mbalimbali.

Hata hivyo kwa upande wake Raphael Maguzo ambaye ni Mstaafu alisema wanafurahishwa na huduma ambazo zimekuwa zikitolewa na Mfuko huo maana aliweza kufungua madai ambao yalifanyiwa kazi kwa wakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...