* Wahitimu watakiwa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya taaluma

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB,) imeshauriwa kuendelea kutoa huduma kwa wateja wao kupitia ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam inayohudumia na maeneo yanayozunguka licha ya kuhamia rasmi makao makuu ya Nchi Dodoma tangu Septemba 30, 2022 ili kuweza kuwafikia watanzania wengi zaidi kwa wakati.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Sera wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB,) Fredrick Mwakibinga katika mahafali ya 11 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB alipomwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba.

"Napenda kuwapongeza wahitimu wote ambao mtatunukiwa vyeti pamoja na shahada za umahiri ila mfahamu kazi kubwa mnayokwenda kuifanya kwa jamii.... Ninaelewa vizuri hatua na changamoto mlizopitia leo mnastahili pongezi....Jitihada zinazofanywa na bodi zinaonekana dhahiri endeleeni kuwahudumia watanzania katika ofisi za hapa Dar es Salaam na Dodoma pia " Amesema Mwakibinga.

Pia Mwakibinga amewapongeza na kuwashukuru wahitimu hao kwa uvumilivu wa kusubiri kuteuliwa kwa bodi ya wakurugenzi na kueleza kuwa Wizara inatambua changamoto iliyojitokeza na tayari imechukua hatua ili changamoto hiyo isijitokeze tena wakati mwingine.

Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PSPTB Jacob Kibona amesema mahafali hiyo ni ya 11 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi 2007 na kueleza kuwa kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Bodi hiyo, matokeo yote ya mitihani ya kitaaluma ya PSPTB ni lazima yapitiwe na kuidhinishwa na bodi ya Wakurugenzi.

"Kwa bahati mbaya kuanzia septemba 2019 hadi novemba 2021 PSPTB haikuwa na bodi ya wakurugenzi baada ya iliyokuwepo awali kumaliza muda wake hali hii ilipelekea kutokufanyika kwa mahafali kwa miaka mitatu napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango hatimaye bodi ya wakurugenzi imeteuliwa Novemba 2021." amesema Kibona.

Vilevile Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Bw. Godfred Mbanyi amewaasa na kuwataka wahitimu hao kufanya kazi kwa kufata maadili ya kitaaluma ili kulinda heshima ya fani hiyo na kuleta ufanisi katika matumizi ya rasirimali za Umma kwa manufaa ya Taifa .

"Tunaposema maslahi aidha mkitumika sekta binafsi au sekta za Umma wote mnahitaji kufanya kazi kwa maadili, Tunahitaji kampuni binafsi zikue kwa kufanya biashara kubwa ili ziweze kulipa kodi na Nchi iweze kuendeleza shughuli za maendeleo katika jamii." Amesema Mbanyi.
Kamishina wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Fredrick Mwakibinga akizungumza katika mahafali ya 11 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB na kuishauri bodi hiyo kuendelea kutoa huduma kupitia ofisini yake ya Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo jirani licha ya kuhamia rasmi jijini Dodoma toka Septemba 30,2022 wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB,) Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa Mahafali ya 11 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB ambapo amewaasa wahitimu kufanya kazi kwa kufata maadili ya kitaaluma ili kulinda heshima ya fani yao na kuleta ufanisi katika matumizi ya rasirimali za umma kwa manufaa ya Taifa wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi PSPTB Jacob Kibona akizungumza katika hafla hiyo na kueleza kuwa mahafali hiyo ni ya 11 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi 2007 nakusema kuwa kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha bodi matokeo yote ya mitihani ya bodi ni lazima yapitiwe na kuidhinishwa na bodi ya Wakurugenzi.
Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Amani Ngonyani akizungumza kwenye mahafali ya 11 ya Bodi hiyo tangu kuanzishwa kwa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi 2007 yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.





Matukio mbalimbali katika picha katika hafla ya Mahafali ya 11 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...