Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Abubakari Kunenge akiwa ameshika fedha kiasi cha Sh.Mil.1 alizowasaidia akinamama wauza chakula wa Mailimoja Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Abubakari Kunenge akizungumza na Waandishi wa Habari  hawapo pichani  leo mchana kwenye viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha.
Diwani wa Kata ya Maili moja Kibaha Ramadhani Lutambi akimsikiliza mwandishi wa habari leo Oktoba 4,2022 Maili Moja Mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wamachinga Mkoa wa Pwani, Philemon  Maliga akizungumza na mwandishi wa habari leo Oktoba 4,2022 Maili Moja Mkoani Pwani.

Na Khadija Kalili, KIBAHA
MKUU wa Mkoa wa Pwani,  Abubakari Kunenge ametangaza kuwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tano Daktari Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgeni rasmi kwenye maonesho ya wiki ya viwanda yanayoanza rasmi kesho Oktoba 5 hadi 10, 2022 yatakayofanyika kwenye viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

RC Kunenge amesema hayo leo mchana Oktoba 4, 2022 alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa Dkt. Kikwete atayazindua rasmi Oktoba 6 mwaka huu.

Aidha RC Kunenge amesema kuwa maonesho hayo yatawashirikisha wawekezaji kutoka katika viwandambalimbali wapatao zaidi ya 200.

Amesema kuwa Oktoba 8 kutafanyika kongamano maalumu la uwekezaji ambalo limepangwa kufanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kwa Mfipa Kibaha ambapo kutakuwa na mijadala inayohusu uwekezaji, uchumi huku mijadala hiyo ikiongozwa na wataalamu wabobevu katika nyanja ya uwekezaji na maafisa biashara,viongozi kutoka katika Taasisi za serikali ambao ndiyo watatoa elimu juu ya uwekezaji ndani ya Mkoa wa Pwani na nchi nzima kwa ujumla pia wananchi wa kada zote watakuwepo na watapata fursa kutoa maoni yao huku lengo kubwa likiwa ni kuongeza kasi ya uwekezaji ndani ya Mkoa wa Pwani.

"Maonesho haya yatatoa taswira ya wepesi na urahisi kwa wawekezaji kuwekeza ndani ya Mkoa wa Pwani ikiwa ni pamoja na kuonyesha utaalamu na teknolojia za kisasa pamoja na kuwasikiliza wawekezaji wenyewe hii ikiwa ni katika kuunga mkono hoja ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mama yetu Samia Sukuhu Hassan katika kuinua uchumi wa nchi" amesema RC Kunenge.

Amesema kuwa Mkoa una vivutio vya utalii 72 na mkoa umejiweke mkakati wa kuvitangaza ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja kuutangaza uchumi wa buluu.

Katika hatua ingine ingine RC Kunenge alipokua akikagua maandalizi ya mabanda kwenye viwanja hivyo Mailimoja Kibaha amewachangia kikundi cha kina mama ambao ni wauz vyakula wa Kibaha kwa kuwapa kiasi cha Sh.Mil.1 ili waweze kujiongezea mtaji pale walipopungukiwa.

"Hakuna urasimu katika kuwekeza ndani ya Mkoa wa Pwani na nchi nzima kwa ujumla hivyo natoa rai kwa mwekezaji yoyote ambaye ana teknolojia yake ama raia ana jambo lake aje atapata nafasi ya kujitangaza usalama upo wa kutosha na niwaombe wakaazi wa Mkoa wa Pwani tujipange kuonyesha ukarimu wetu kwa wageni wetu watakaofika na kutumia fursa hii kujitangaza kwani idadi ya wawekezaji imeongezeka".

Anneth Stanford ambaye ni mpika chips amezungumza kwa niaba ya wenzake ametoa shukrani kwa RC huku wenzake wakipiga vigeregere vya kumshangilia huku wakimuombea kwa mungu amzidishie pale alipotoa na kuwa Rais Samia hakukosea kumleta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Naye Diwani wa Kata ya Mailimoja Ramadhani Lutambi ametoa shukrani zake kwa uongozi wa Mkoa kutokana na kutoa fursa adhimu kwa wakaazi wa Kibaha huku akiwahimiza kujitokeza kwa wingi na wachangamkie fursa hiyo waliyopewa na Mkuu wa Mkoa kwani alikua na uwezo wa kwenda eneo lolote ndani ya Mkoa wa Pwani.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa Pwani Philemon Maliga amesemakuwa tayari amesha wahimiza wamachinga ndani ya Mkoa kila mmoja aiweze kunufaika na fursa hii.

Jumla ya wawekezaji 200 wamethibitisha kushiriki amesema RC Kunenge.
Amesema kuwa maonyesho haya yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na SIDO ambapo pia itahusisha Kanda ya Kusini Mashariki inayoundwa na Mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani yote itahusika kwenye maonyesho hayo" amesema RC Kunenge.

Maoneesho haya yanafanyika kwa mara ya tatu ambapo kwa mwaka huu yameongezeka ubora kutokana maandalizi makubwa na mahusiano mazuri kati yao na wawekezaji kwa ujumla wamepata mwamko." Amesema RC Kunenge.

Amesema kuwa mbali ya viwanda, ufugaji, uwindaji wa kibiashara , utalii , pia Mkoa wa Pwani una madini mengi bila kusahau fursa ya uvuvi hivyo wananchi na wazawa wa ndani na nje ya nchi wote wanakaribishwana kuongeza kuwa Mkoa una viwanda zaidi ya 1460 huku idadi ha viwanda vikubwa ni 90 .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...