Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa Msaada wa mahitaji muhimu kwa mama waliojifungua watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni, Kigoma.
Mahitaji hayo yamekabidhiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Jengo la kutolea Huduma za Wagonjwa wa Dharura (EMD) na Wagonjwa wa uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma. Leo tarehe 18 Oktoba, 2022.
“Rais Samia amewashika mkono Mama waliojifungua Watoto njiti kwa kutoa Mashuka, blanket, Vitenge, Sabuni, pampasi, mafuta ya nywele na mahaitaji mengine ikiwa ni pamoja ba vyakula kama Mchele na Sukari” Amesema Waziri Kairuki.
Kwa upend wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali italeta Vifaa tiba kwa ajili ya kuhudumia Watoto njiti ikiwa ni pamoja na Mashine za Kufua hewa ya Oksijeni, Mashine za Kuzalisha hewa joto na Mashine za kutunza Watoto njiti.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni, Dkt. Stanley Binagi amesema vifaa tiba na Mahitaji hayo yatasaidia utoaji wa huduma bora kwa Watoto Njiti waliopo na wanaoendelea kuzaliwa katika Hospitali hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...