Wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro wametakiwa kutunza maji kitokana na upungufu wa maji kwenye mto Ruvu unaotoa Huduma za Majisafi katika Mikoa hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amosi Makalla alipotembelea na kujua hali ya uzalishaji maji akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Bodi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

Makalla amesema kina cha majibhasa huku kwenye vyanzo vya uzalishaji wa maji kimeshuka kwa maana hiyo kutakuwa na upungufu wa maji kwa kiasi kikubwa kwa Mikoa hiyo.

 "Tilitarajia mvua za mwezi wa Tisa na kumi kuwepo mvua za vuli ambazo zinakuja kusaidia kuongeza maji kwenye hivi vyanzo maji na pia kuna taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa kuwa kitakuwepo na upungufu wa mvua na kuwepo kiangazi cha mda mrefu na ndo maana tumeshindwa kupata mvua za vuli.

Pia amesema kuwa Serikali pamoja na Bodi ya DAWASA kuna jitihada zimefanyika kwanza hiki kinachopatikanika kinatumika vizuri lakini pia kamati zote za kamati za ulinzi na usalama za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro zimeweza kutimiza majukumu yake kwa wale wote wanaochepusha maji wanachukuliwa hatua ili kuweza kuongeza upatikani wa maji kwenye mto Ruvu.

"Hakuna kisingizio kingine chochote cha kina cha maji zaidi ya utegemezi wa mvua na hapa nasisitiza kuwa Serikali inafanya jitihada kwa hiki kidogo kilichopo kinawafikia wananchi na asije mtu akasema hata mvua inaweza kuletwa na Serikali." amesema Makalla

Pia Makalla amewataka DAWASA kumaliza kwa haraka mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kuweza kupunguza makali ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam pamoja na Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amosi Makala akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam  pamoja na Bodi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kutembelea na kujua hali ya uzalishaji maji Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amosi Makalla, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam  pamoja na Bodi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)  wakipata maelezo kuhusu hali ya uzalishaji wa maji katika chanzo cha maji ya Ruvu Juu kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa ziara ya kutembelea na kujua hali ya uzalishaji maji Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amosi Makala, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam  pamoja na Bodi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakiendelea  kufanya ziara ya kutembelea na kujua hali ya uzalishaji maji Jijini Dar es salaam.
Muonekano wa maji kwenye mto Ruvu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...