Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza na walimu, wazazi na wanafunzi wa shule ya Msingi Mkoani iliyopo ilala boma jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea takribani madawati 100 yaliyotolewa na Klabu ya Rotary ya Dar es salaam ambayo inafanya kazi ya kujitolea Kwa jamii.
Jumla ya Madawati 100 yaliyotolewa Leo octoba mosi na Klabu ya Rotary ya Dar es salaam kama sehemu ya mchango wao Kwa jamii katika shule ya Msingi Mkoani iliyopo ilala boma wilaya ya ilala jijini Dar es salaam na kupokelewa na Mkuu wa wilaya hiyo

Na Khadija Seif, Michuzi Tv
KLABU ya Rotary ya Dar es Salaam, imekabidhi madawati 100 kwa shule ya msingi Mkoani iliyopo Ilala jijini Dar ikiwa ni sehemu ya madawati zaidi ya 1,500 yenye thamani ya Sh. Milioni 240 ambayo yameshatolewa na klabu hiyo kwa shule mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza jijini Dar es salaam Octoba Mosi wakati wa kupokea Madawati hayo Mkuu wa wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija amesema mchango huo ni muhimu sana kwani serikali inafanya jitihada kubwa kuimarisha elimu hivyo mchango wa wadau kama Rotary ni muhimu sana ili kuharakisha maendeleo katika sekta ya elimu.
''Serikali inathamini sana michango inayotolewa na wadau mbalimbali mashuleni kwani inasaidia moja ya Majukumu ya Serikali na jamii kwa ujumla kutengeneza Mazingira rafiki kwa wanafunzi hivyo klabu ya Rotary imesaidia kunyanyua wanafunzi zaidi ya elfu 4 waliokua wakiketi sakafunu badala yake Mchango wa Madawati umekua mkombozi Kwa wanafunzi hao".
Mkuu huyo wa wilaya ameiomba klabu ya Rotary kuendelea kushirikiana na serikali na ameahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Rotary na wadau wengine katika kuimarisha huduma za jamii .
Pia ameuomba uongozi wa shule ya Msingi Mkoani kuhakikisha wanatunza madawati hayo na kuhakikisha wanafanya ukarabati wa haraka pale ikitokea dawati limeharibika .
Rais wa klabu hiyo Nikki Aggarwal, amesema klabu hiyo imekuwa ikishirikiana na jamii ili kuboresha huduma za jamii.
Aggarwal amesema bado wanaendelea na mradi wa kutoa madawati ambapo unaenda sambamba na zoezi la upandaji miti ili kuhifadhi mazingira.
Aidha, amesema Klabu ya Rotary ni jumuiya ya watu zaidi ya milioni moja kote duniani wenye lengo la kusaidia jamii zenye uhitaji na haita sita kuendelea kuisaidia jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...