Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba (kulia) akikagua bidhaa katika Banda la Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC alipozindua Maonesho katika Siku ya Mbolea Duniani, katika Viwanja vya Kimondo Mlowo, wilayani Mbozi,mkoani humo. wa pili kushoto ni Kaimu Meneja wa TFC, Kanjel oba na wa pili kulia no Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji Mbolea ya SBL Joe Kiriuki kutoka nchini Kenya
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya utengezaji mbolea ya SBL Joe Kariuk kutoka Kenya akizungumzia na vyombo vya habari kuhusu kugawa bure mbolea hiyo kwa wakulima katika maonesho hayo
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya utengezaji mbolea ya SBL Joe Kariuk kutoka Kenya akizungumzia na vyombo vya habari kuhusu kugawa bure mbolea hiyo kwa wakulima katika maonesho hayo
NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya utengenezaji na usambazaji wa mbolea kutoka nchini Kenya SBL imetangaza neema kwa wakulima hapa nchini ambapo itatoa mfuko mmoja bure kwa wakulima watakaofika katika Banda lake katika maonesho ya Siku ya Mbolea Duniani yanafanyika kitaifa katika Viwanja vya Kimondo,Mlowo,Wilayani Mbozi, mkoani Songwe.
Akizungumzia na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Joe Kariuk, amesema watakaonufaika na ofa hiyo ni wakulima watakao fika katika Banda la Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na kununua mifuko kuanzia mitatu ya mbolea ya SBL Kisha kupewa mfuko mmoja bure.
Joe amesema SBL dhamira ni kuunga mkono jitihada za serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kumwinua mkulima wa kitanzania.
"SBL imeonesha ufanisi mkubwa nchini Kenya. Sasa tunataka hata hapa Tanzania wakulima wanufaike nayo na kwa kuanzia tunatoa mfuko mmoja wa kilo 25 bure kwa wateja watakaofika katika maonyesho haya hapa Songwe,"alisema Joe.
Amesema SBL kupitia TFC imeingiza mifuko 2500 ya mbolea hiyo ya organic ambayo ni rafiki wa mazingira.
"Mifuko hiyo 2500 imeingia Songwe na tutauza na kuigawa bure. Wananchi waje katika uwanja wa Kimondo Mlowo na wafike katika Banda la TFC" ameongeza Joe.
Awali Kaimu Meneja wa Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC Kanjel Mloba alisema mbolea hiyo ya SBL imeingizwa nchini kutokana na ubora wake na ufanisi huko Kenya.
"Pamoja na mbolea nyingine leo katika maonesho haya TFC Tumetambulisha mbolea hii ya SBL ambayo ni organic. Ni mbolea nzuri na tunahimiza wakulima kuitumia"amesema Kanjel.
Amesema TFC itaendelea kuhakikisha inawasaidia wakulima kuwafikishia mbolea bora ili kilimo chao kiwe chenye tija.
Maonesho hayo ya Siku tatu yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRA yameanza leo na yanatarajiwa kufungwa na Wazirii wa Kilimo Hussein Bashe Oktoba 13 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...