Dar es Salaam, Oktoba 27, 2022 – Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua programu
ya kupambana na unywaji wa pombe kwa watu wenye umri mdogo inayolenga kudhibiti tabia ya
unywaji pombe miongoni mwa watoto waendao shule.
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye kundi la watu wenye umri mdogo wa
wanaotumia pombe. Utafiti uliofanywa mwaka 2019 katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro
ulibaini kuwepo kwa mwenendo wa matumizi ya pombe miongoni mwa wanafunzi wa shule za
sekondari wenye umri wa miaka 15 na zaidi ni kutoka asilimia 12.9 miongoni mwa wasichana
mkoani Mwanza hadi asilimia 63.9 miongoni mwa wavulana mkoani Kilimanjaro.
Mwenendo wa matumizi ya pombe miongoni mwa wanafunzi wenye umri wa miaka 13-15 jijini
Dar es Salaam yalikuwa asilimia 5.6.
Kampeni hiyo iliyopewa jina la SMASHED, ni kampeni ya kupambana na unywaji wa pombe ya
SBL, inayotumia michezo ya kuigiza ya jukwaani inayowapa uezofu wa kipekee na kusisimua.
SMASHED hufanyika mashuleni na huelimisha wanafunzi wa sekondari kuhusu madhara ya
matumizi ya pombe katika umri mdogo, kwa kuwashauri kujiepusha na matumizi ya pombe
kabla ya kukomaa.
"Mpango huu unahusisha utoaji wa mafunzo muhimu juu ya athari mbaya za unywaji pombe
katika umri mdogo kwa vijana na jamii. Programu inachanganya matumizi ya maonyesho ya
maigizo na ushiriki wa wanafunzi katika mazingira ya motisha ya kujifunza ili kuwapa ukweli,
ujuzi na ujasiri wa kufanya uchaguzi wa kuwajibika na kuendeleza mitazamo ya uwajibikaji
katika masuala yanayohusiana na afya," alisema Rispa Hatibu, Meneja Mawasiliano wa SBL.
Alisema mpango huo utatekelezwa nchi nzima mwaka huu kwa awamu kuanzia Dar es Salaam
na Mikoa ya Tanga. Zaidi ya wanafunzi 15,000 wamepangwa kufikiwa na mpango huo katika
Mikoa hiyo miwili.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Henry James ambaye aliipongeza SBL
kwa kuja na mpango mzuri wa kukabiliana na tatizo la unywaji wa pombe miongoni mwa vijana
wenye umri mdogo. "Uingiliaji huu ni wa wakati muafaka na utaenda sambamba katika kusaidia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...