Na Pamela Mollel,Arusha
Serikali Mkoa Arusha imeanza mkakati maalumu wa kutenga maeneo ya kuhifadhi wagonjwa wa ebola endapo watatokea kutokana na kuripotiwa ugonjwa huo kuwepo nchi jirani
Akizungumza katika kikao cha afya ya msingi kilichoshirikisha Viongozi na wadau wa afya jijini Arusha Mkuu wa Mkoa Arusha John Mongella amewataka wataalamu wa afya kutoa elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa wa Ebola na namna ya kuchukua tahadhari
Mongella alisema kuwa wananchi wakipewa elimu ya kutosha itasaidia wao kuchukua tahadhari kabla ya hatari
"Hii elimu pelekeni vijijini wananchi huko hawana uelewa juu ya uwepo wa ugonjwa wa hatarii wa Ebola "alisema Mongella
Kwa upande Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt Sylvia Mamkwe alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili kwa kina namna ya kuchukua tahadhari endapo ugonjwa huo utaingia nchi
Amesema kwa sasa hakuna mgonjwa aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa huo hatari na serikali inaendelea kuchukua hatua namna ya kukabiliana nao
Aidha mamkwe alisema jumla ya watumishi 122 wa afya wameandaliwa kutoa elimu katika maeneo mbalimbali vijijini
"Kwa sasa tunakabiliwa na changamoto ya vifaa ila serikali inapambana kuhakikisha inapata vifaa vya kukabiliana na ugonjwa huo"alisema Mamkwe
Dalili za ebola ni kutoka kwa damu maeneo mbalimbali ya mwili kama vile masikioni,mdomono,puani


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...