MKUU wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa amemkabidhi Tuzo ya Heshima kama Kiongozi Kijana wa mfano Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC ya Chama Cha Mapinduzi CCM,Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika utumishi.

Mwasa amemkabidhi Shaka tuzo hiyo mbele ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama na Serikali Mkoa wa Morogoro wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo kwa Mkoa huo uliofanyika wilayani Kilosa Oktoba 4,2022 na kuhudhuriwa na viongozi wa Chama na Serikali pamoja na wananchi.

"Leo umeshiriki nasi katika kuzindua msimu wa kilimo ambapo tumepanda pamoja Mkonge kwenye Shamba la vijana lenye ukubwa wa ekari 78,tunakushukuru sana na tutakikisha mche uliopanda unakuwa mche bora kwenye Shamba lile .

Sambamba na uzinduzi wa msimu tuko hapa kwenye mkutano huu ikiwa ni kilele msimu wa kilimo mkoani Morogoro,kauli mbiu yetu imekuwa tunaanzia shambani, Ajenga 10/30 kilimo ni Biashara tunaanzia Shambani.Kwanini kilimo tumeweka nguvu kubwa kwenye kilimo kwasababu asilimia 65 ya wananchi wa Morogoro ni wakulima, kwa hiyo tunapogusa kilimo tumewagusa asilimia 65 ya wananchi wa Morogoro.

"Tumeaandaa tuzo kwako Meshimiwa mgeni rasmi ,siku ya uzinduzi wa Marathon tulitoa zawadi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na utamfikisha salamu kwamba tuzo yake inakuja kupitia mfumo rasmi. Lakini nawe leo unapewa tuzo rasmi."alisema Mkuu wa Mkoa Fatma Mwasa.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...