Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi akipokea kifaa tiba - mashine ya Ultrasound kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania Mrisho Yassin katika hafka iliyofanyika leo Hospitalini hapo Jijini Dar es Salaam
KATIKA kuhakikisha sekta ya afya inazidi kukua na jamii ya watanzania inakuwa na afya bora kampuni ya Swissport Tanzania PLC imeendelea kuwa karibu na jamii na kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Sama Suluhu Hassan kwa kutoa msaada wa kifaa tiba ‘Ultrasound’ chenye thamani ya shilingi milioni 68 katika taasisi ya CCBRT.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania PLC Mrisho Yassin amesema mchango huo umeelekezwa kuwasaidia akina Mama wajawazito.
‘’Tunatambua kuna changamoto ya vifaa tiba na sisi kama kampuni tumeliona hili na kuona kutoa mchango huu, kwa taarifa tuliyopewa kifaa hiki kitasaidia sana kutokana na uhiitaji wa mashine hii hapa CCBRT ili kusadia jamii ya watanzania akina Mama wajawazito.’’ Amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi ameishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kuchangia kifaa tiba hicho cha Ultrasound kitakachoongeza nguvu ya kuwahudumia akina Mama wajawazito wengi zaidi na kwa ufasaha.
‘’Sisi kama CCBRT asilimia 87 ya wagonjwa wanaokuja hapa ni aidha wanapata huduma za bure kabisa au wanachangia….Tunahitaji kushikwa mkono katika maeneo makuu matatu ya huduma za kibingwa na bobezi za afya, mafunzo kwa wafanyakazi na watoa huduma na eneo la vifaa na vifaa tiba na tunawashukuru Swissport na tuendeleze uhusiano huu.’’ Amesema.
Amesema, tangu kuanza kutolewa kwa huduma katika kitengo cha Mama na Mtoto mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu wamewahuduma akina Mama wapatao 225.
‘’CCBRT tunatoa shukrani zetu za dhati kwa SwissPort kwa kututembelea na kutoa kifaa hiki kwa umoja huu iko siku ambayo tutaona kila mwanamke anayepata ujauzito anajifungua salama na kwa furaha….Tunashukuru sana kwa msaada wenu na ushirikiano wenye kwenye huduma hizi za kuokoa maisha ya watu.’’ Amesema.
Aidha amesema, mwezi Julai mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu alizindua rasmi kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto ambacho kimepewa jina la ‘CCBRT- Samia Suluhu Hassan Maternity Wing’ kutokana na juhudi binafsi na Serikali anayoiongoza katika kupigania afya za akina Mama wajawazito na watoto wachanga pamoja na maboresho makubwa ya sekta ya afya nchini kote.
‘’Lengo la kuanzishwa kwa kitengo hiki ni cha uzazi ni kutaka kuwahakikishia akina Mama wote uzazi salama, kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi sambamba na kuzuia ulemavu….kitengo hiki kimedhamiria kuwahudumia akina Mama wajawazito wenye ulemavu, wenye historia hatarishi za uzazi, akina Mama wenye historia ya fistula na mabinti wanaopata mimba katika umri mdogo.’’ Amesema.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya ukabidhiwaji wa Kifaa tiba cha Ultrasound kwa ajili ya Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto kwenye hospitali hiyo kutoka kampuni ya Swissport Tanzania chenye thamani ya Milioni 68.
Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania Mrisho Yassin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi kifaa tiba cha Ultrasound kwa ajili ya Kitengo cha Afya ya mama ma mtoto katika Hospitali ya CCBRT leo Jijini Dar es SalaamMuonekano wa kifaa tiba 'Ultrasound'
.jpeg)
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Swissort Tanzania mara baada ya makabidhiano ya kifaa tiba cha Ultrasound kilichotolewa kwa ajili ya Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto kwenye hospitali hiyo kutoka kampuni ya Swissport Tanzania chenye thamani ya Milioni 68.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...