Na Abdullatif Yunus MichuziTV - Kagera
Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe. Murshid Ngeze (Diwani wa Rukoma) yupo Nchini Korea Kusini, katika Ziara ya Kikazi ambapo mapema asubuhi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Lucy Slack juu ya kufungua Ushirikiano Kati ya Jumuiya ya Madola na ALAT, Bi. Lucy amekubali na ameahidi kutembelea Tanzania Mwezi Novemba Mwaka huu.
Kwa wakati Mwingine Pia Mhe. Ngeze Mchana amesaini Mkataba wa ushirikiano katika Maendeleo na Rais wa Jumuiya ya serikali za mitaa Nchini Morocco Mhe. Fatna Elk Hiel. Mkataba huo ni wa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wilaya Bukoba na Halmashauri ya Arbaoun nchini Morocco unaolenga kwenye Sekta ya Kilimo, utawala katika sSerikali za mitaa, miundombinu, makazi n.k.
"..Tumekubaliana wataalamu wa pande zote mbili waandae mipango na tujadili ipi ya kuanza nayo.." Amesema Ngeze
Ziara hiyo ya Mhe. Ngeze inaendelea Mwezi huu mwishoni ambapo amealikwa Nchini Morocco kusaini kwa ajili ya Tanzania nzima (ALAT) Katika kusaini alikuwepo Barozi wa Morocco nchini Korea,waziri wa mambo ya nje wa Morocco na maafisa mbalimbali kutoka Morocco
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...