Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Dkt. Michael Ng’umbi, amewataka wadau wa elimu nchini kufanya kazi kwa ufanisi ili kuwezesha Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari kwa njia Mbadala (SEQUIP-AEP) kuwa wa mafanikio.

Dkt. Ng’umbi ameyasema hayo leo tarehe 3 Oktoba, 2022 wakati wa ufunguzi wa warsha ya uhamasishaji na uzinduzi wa mwongozo wa uendeshaji wa Elimu ya Sekondari kwa njia mbadala iliyofanyika jijini Tanga na kuhusisha maafisa wa elimu ya watu wazima,wakuu wa Shule na wathibiti ubora wa elimu kutoka katika mikoa 26 Tanzania Bara.

Amesema TEWW imejipanga vyema katika kuhakikisha mradi huo unaolenga kuwapa fursa ya masomo wasichana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 21 waliokatisha masomo ya elimu ya sekondari kwa sababu mbalimbali unafanikiwa.

“Serikali kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kwa kushirikiana na wadau wengine imejipanga kuhakikisha mradi wa kuboresha ubora wa elimu kwa njia mbadala unafanikiwa na kutatua changamoto zote zinazokabili utoaji wa elimu hiyo,”amesema.

Kwa mujibu wa Dkt. Ng’umbi, hadi sasa TEWW imefanikiwa kudahili wasichana 3,333 nchini ambako mkoa wa Mbeya umeongoza kwa kudahili wasichana 468 kwenye vituo 12 na kufuatiwa na Mwanza ambako wasichana 280 wamedahiliwa kwenye vituo 14.

Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Sedet Bulaya, amesema kuwa TAMISEMI itasimamia kwa karibu utekelezaji wa mwongozo wa uendeshaji wa Elimu ya sekondari hasa kwa kuzingatia kuwa TAMISEMI ndiyo iliyopewa dhamana ya usimamizi wa miundombinu ya kutekeza miradi ya elimu nchini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...