Na Mwandishi Wetu,
LEO Oktoba 11 mwaka 2022, Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Shirika la UNESCO umeshiriki katika hafla ya utoaji wa tuzo maalum.
Utolewaji wa tuzo hizo umefanywa kwa Taasisi za 'Girls Livelihood and Mentorship Initiative' (GLAMI) kutoka Tanzania na 'Room to Read' kutoka Cambodia ili kutambua mchango wao katika kuimarisha utoaji wa elimu kwa wasichana na wanawake. Tuzo hiyo inayofadhiliwa na China imetolewa kwa Taasisi hizo mbili.
GLAMI ni Taasisi inayofanya kazi nchini kuanzia mwaka 2001 kwenye mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kwa lengo la kutoa elimu ya maisha (life skills) kwa wasichana wanaoingia sekondari ili kuongeza ufaulu na pia kuwaandaa kwa ajili ya masomo na maisha ya chuo kikuu.
Imeelezwa kwamba juhudi hizo zimewezesha taasisi hiyo kufuzu kwenye mchakato uliohusisha waombaji 75 kutoka nchi 48 duniani.
Aidha, wakati wa kupokea tuzo hiyo Devotha Mlay ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Miradi ya GLAMI, amemshukuru Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kukuza elimu ya wasichana na wanawake.
Na kwamba nafasi yake kama mwanamke wa kwanza aliye Rais nchini Tanzania kumewahamasisha wasichana wengi kuweka mkazo kwenye elimu ili kufikia malengo yao.
Home
HABARI
UBALOZI NA UWAKILISHI WA KUDUMU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UNESCO UMESHIRIKI HAFLA UTOAJI TUZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...