Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ameeleza lengo la ongezeko la idadi ya watalii milioni 5 na kuzalisha dollar za kimarekani Bilioni 6 ifikapo,2025 itawezekana kutokana na ongezeko la watalii kwa sasa.

Akitembelea baadhi ya mabanda ya washiriki wa maonyesho ya wiki ya biashara na uwekezaji Mkoani Pwani yanayofanyika Mailmoja Kibaha Mjini,Ulega akiwa banda la Wizara ya Utalii pamoja na banda la Halmashauri ya Mafia na Mkuranga alisema ,namna idadi inavyoongezeka na kuingiza dollar bilioni sita kufikia 2025 inawezekana .

"Inabidi tushirikiane ,tufanyekazi ,tuwe wabuni ,umoja na kupanua wigo wa kujitangaza ili kuongeza watalii nchini na kuinua Pato la Taifa hadi lifikie asilimia 30-40 na hii kwa juhudi zetu Tutafika"Hakuna kinachoshindikana inawezekana."alifafanua Ulega.

Ulega alieleza ,Hifadhi za Taifa ikiwemo Ngorongoro,Saadan ,Selou,na Vikindu Forest zifanye kazi ili kuvutia watalii ndani na nje ya nchi.

Aidha akitembelea Banda la Halmashauri ya Mkuranga aliwataka kufanya marejesho ya tamasha la Utalii Mkuranga ambalo lilileta matokeo chanya.

Ulega alifafanua kwamba ,Vikindu forest iliyopo Mkuranga ni utalii tosha ambapo kwasasa watalii 500 wanafika kujionea vivutio mbalimbali na wengine kwenda kupumzika kwa mwezi .

"Hii ni hatua nzuri ya uwekezaji endeleeni kupaendeleza ili kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje "

Wakati akiwa Banda na Halmashauri ya Mafia ,Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mohammed Hussein aliwashawishi watu waende Mafia kujionea kivutio kikubwa Cha Papa Potwe.

Ameeleza wavuvi wa maeneo jirani Kama Zanzibar wanaenda ambao wanaenda kwa ajili ya samaki huyo ambae ni kivutio kwao.

"Samaki hawa hupatikana maeneo machache duniani, na kwa mujibu wa tafiti za bahari ni miongoni mwa viumbe vilivyopo hatarini kutoweka, Moja ya maeneo wanayopatikana ni kisiwani Mafia Tanzania, sehemu nyingine ni kama Mexico na Philipenes."alibainisha Hussein.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...