NA STEPHANO MANGO, SONGEA

MWENYEKITI wa Uvccm Songea Mjini  Mwl Joachim Komba akiwa  Mgeni rasmi katika sherehe za mahafali kwenye shule ya msingi Luhirakati ameongoza harambee ya kuchangia manunuzi ya computer kwaajili ya kurahisisha ufanisi katika utendaji wa kazi shuleni apo.

Katika Harambee hiyo kiasi cha shilingi laki nne thelathini na mbili elfu (432 000/-)  kilipatikana ambapo Mwenyekiti wa Uvccm Songea Mjini  Mwl Joachim  Komba alichangia kiasi cha shilingi laki moja (100 000/-) kama salamu za wana Uvccm Songea Mjini

 Sambamba na kiasi hicho pia alitoa mifuko miwili ya mbolea itakayotumiwa katika shamba la shule hiyo

Komba hakuishia hapo aliwakumbuka wanafunzi wapenda michezo kwa kuwapa mipira miwili ikiwa mmoja wa football na mmoja wa netiboli

Aidha Mwenyekiti huyo ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi wa kata ya Mwengemshindo ni jinsi gani CCM kupitia Rais wa JMT Mama Samia Suluhu Hassani  inavyopambana kutatua kero za wananchi

Mwenyekiti huyo ameainisha juhudi mbalimbali za serikali ya awamu ya sita zikiwemo, Kutatua kero ya madarasa kwa kujenga madarasa sita katika kata hiyo

Pia kuondosha ada kwa shule za advance na Kuondosha ada za mitihani kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita na kufanya dhana ya elimu bila malipo kutimia kwa mama

Alieleza pia kutoa rudhuku kwenye mbolea na sasa mkulima anapata mbolea kwa nusu bei na kuahia  ruzuku za mafuta  petroli, dizeli, acha nafasi za ajira kila leo

Mwenyekiti  huyo alipata wasaa wa kuzungumza na kuchangamana na wanafunzi na kuwakaribisha katika Umoja wa vijana CCM kama Chipukizi wa chama ili walelewe na wapikwe waje kua viongozi bora wa chama na serikali

Aidha Mwenyekiti wa Uvccm Songea Mjini  Komba ameushukuru uongozi wa Shule hiyo kwa kutambua umuhimu wa UVCCM kwa Mwaliko huo na kuahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika kila jambo.

Kwa upande wake Anna Milanzi ambaye ni mmoja wa walimu katika hule hiyo alishukuru michngo hiyo iliyotolewa na Mgeni rasmi kwani itakuwa chachu katika kuendeleza vipaji na elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...