Vyama vya kisiasa na asasi za kiraia vimetakiwa kuwaelewesha vizuri wanachama wao kuhusiana na dhana nzima ya bima ya afya kwa wote.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka wizara ya afya Bw. Edward Mbanga wakati wa semina ya kuwajengea uelewa viongozi mbalimbali kutoka vyama vya kisiasa na azaki za kiraia katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Bw. Mbanga amesema Serikali inataka wananchi wengi kuchangia bima ya afya kwa wote ili kuweza kuwasaidia wale wachache wenye matatizo ya kiafya kupata matibabu kupitia mfumo huo.

Amesema kuanzishwa kwa mfumo huo utahakikisha wananchi watapata huduma za afya kwenye vituo vya afya kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa.

"Wananchi watakaojiunga kwenye mfumo huo, watapata huduma bora kwani hivi sasa Serikali imeweza kuboresha miundombinu kwenye vituo vyake pamoja na kuwekeza kwenye vifaa tiba .

Kwa upande wa udhibiti wa huduma na fedha Bw. Mbanga amesema Serikali inaweka mfumo thabiti wa kusimamia mifuko ya bima ya afya na kwamba ipo katika utaratibu wa uchambuzi wa kina ili kila taasisi itakayosimamia iweze kutekeleza kwa ukamilifu pasipo upungufu wowote.

Hata hivyo amewashukuru washiriki hao na kuahidi kupokea maoni yote yakiyowasilishwa na kuyafanyia kazi ipasavyo ili kuboresha muswada ili uweze kukidhi mahitaji ya wananchi.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...