Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

WAKAZI wa Buguruni Kisiwani, Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es salaam wametuma Salamu maalum kwa Jeshi la Polisi kupitia kwa IGP. Camillius Wambura wakimtaka aendelee na Operesheni za kuwakabili Wahalifu hususani Panya Road ambao wamekua wakihatarisha maisha yao.

Wananchi hao wamesema hayo wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Ghana iliyopo Buguruni kisiwani ambapo walitoa maoni yao kuhusiana na namna Jeshi la Polisi walivyojitoa kupambana na Panya Road na kutumia muda huo kutuma salamu maalum kwa IGP. Wambura.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Omari Kumbilamoto amewaambia sababu kubwa ya kuwepo PanyaRoad ni wazazi kutowasihi watoto wao kusoma licha ya jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye utoaji wa Elimu Bure, hivyo amewataka kumuunga mkono Rais Samia kuitikia wito wake wa kuwapeleka shule.

Kumbilamoto ameongeza kuwa Wananchi washirikiane vizuri na Jeshi la Polisi wasibeze juhudi hizo badala yake wajikite katika kutoa mawazo na maoni namna gani wahalifu hao waliobakia watatiwa kwenye mikono ya sheria.

"Kipekee niwashukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Amos Makala pamoja na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Jumanne Murilo kwakweli wamefanya kazi kubwa sana ilifikia mahala ndugu zetu Waislam walikuwa hawawezi kwenda kuswali swala ya alfajiri kwasababu ya kuhofia na Wakristo vilevile walikuwa hawawezi kuwahi ibada ya asubuhi sababu ya kuhifia usalama wao".

Aidha Mwenyekiti wa Mtaa huo Mh Uwesu Bakari amewataka wazazi kushirikiana na jeahi la polisi endapo mzazi atabaini mtoto wake amekamatwa kwa tuhuma za uhalifi aweze kumuacha kwanza ajifinze maadili na sio kukimbilia kumtolea zamana ambapo wakirudi mtaani wanarudia sababu hawajakaa kwa muda mrefu ili abadilishe tabia.

"Namshukuru sana Polisi Kata vijiwe vyote hapa anaingia lakini mtu akikamatwa dakika mbili mzazi anaenda kituoni kwenda kumtoa kwa kufanya hivi Jeahi la Polisi munalivunja nguvu muache akae asiyefinzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu" amesema Mh Uwesu.

Mmoja ya wahanga wa panya road wa Mtaa huo wa Kisiwani aliejitambulisha kwa jina la Prisca Masanja amepongeza Serikali na Jeshi la Polisi kwa kuweza kurudisha amani katika Mtaa huo na kusema kuwa panya road ni wauwaji na kuwataka wazazi ambao wamewaficha watoto wao ndani wawasalimishe kituo cha Polisi .

"Nipo tayari na nimejitoa muhanga kwa lolote Ili kuhakikisha wahalifu "panya road wanakamatwa tumechoka manyanyaso na mauaji tumepoteza vingi kutokana na kutokutoa kwetu ushirikiano wa awali kwa jeshi la Polisi badala yake tumekaa kulalamikia Serikali yetu ya Mtaa na viongozi wake. Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Omari Kumbilamoto akizungumza na Wananchi wa Kata ya Buguruni kisiwani (Ghana) na kuwaasa wazazi kuhakikisha wanalea watoto kwenye maadili mema Ili kupunguza vitendo vya uhalifu Huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano zaidi kwa Jeshi la polisi kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu waliobakia



Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguruni kisiwani (Ghana) Uwesu Bakari akifungua rasmi kikao na wananchi wa kata hiyo Ili kutoa uelekeo uliopo ambavyo Jeshi la Polisi lilivokabiliana na wahalifu "panya road" kikao hicho kilichofanyika Shule ya Msingi Ghana iliyopo Buguruni kisiwani jijini Dar es salaam

Wananchi waliojitokeza katika hadhara iliyofanyika katika Shule ya Msingi Ghana iliyopo Buguruni kisiwani jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupongeza Jeshi la Polisi pamoja na kutolea ufafanuzi wa mauaji ya wahalifu "Panyaroad" na mikakati ya kuboresha Kata hiyo kupambana na uhalifu
Mmoja ya wananchi kutoka Kata ya Buguruni kisiwani (Ghana) Prisca Masanja akiwasilisha pongezi zake Kwa jeshi la Polisi baada ya kurudisha amani katika Mtaa huo mara baada ya kuuwawa Kwa panya road


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...