Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye amezindua  Stampu ya Pamoja yenye historia ya Tanzania na nchi ya Oman, wakati wa  kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 Oktoba mwaka 2022 yenye Kauli Mbiu ya Posta kwa kila mtu. 

Sambamba na hilo  Waziri Nape amezindua mfumo mpya wa Posta Kiganjani ambao utabeba huduma  zote za shirika la Posta na kuziweka mahali pamoja ndani ya simu ya kiganjani.

Akizungumza wakati Uzinduzi huo uliofanyillka Leo jijin dar es Salaam Waziri  Nape amesema Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia imejipanga kuwawazesha watoa Huduma za  posta kuwafikia wananchi Kwa urasi bila kufika Katika ofisi za posta.

"Hili litawezekana kwakuwa Serikali imekalisha utekelezaji wa mfumo wa Anuani za Makazi ambao ni miundombinu Muhimu Katika utoaji wa Huduma" amesema Waziri Nape.

Pamoja na Hayo Waziri Nape amesema historia ya Oman na Tanzania ni ndefu na imezunguka sana ni muhimu historia hii ikalidwa na wao shirika la posta wameamua kulinda  historia hiyo.
Pia waziri amewapongeza viongozi wa shirika la Posta wa Tanzania na Oman Katika kushirikiana na kuzindua stempu ya Pamoja.
Hata hivyo Waziri  ameto wito Kwa  shirika la Posta kuongeza Nguvu Kwenye kubuni biashara nyingine za kiposta zinazoenda na matuzi ya Technolojia Ili kukithi mahitaji mapya ya wateja.

Aidha Waziri Nape amemkabidhi  Mshindi wa Uandishi wa Makala, Bi. Jacqueline J. Liana mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Posta.
"Waziri  Nape amewasihi wa Watanzania kutumia Huduma za posta ambazo zimeboreshwa kwakuwa posta ya Sasa si barua tuuh ni Zaid ya barua" amesema Waziri Nape.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 Oktoba 2022, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Matukio mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 Oktoba, 2022, katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).
Mgeni Rasmi ni Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (mb)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akiwa na Viongzi mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022. Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrise Mbodo akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso, akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...