Njombe
WANAFUNZI 963 waliokuwa wanasoma kidato cha pili katika shule za sekondari mkoani Njombe wameshindwa kufanya mitihani yao ya kidato cha pili kwa mwaka wa 2022/2023 kutokana na utoro pamoja na sababu nyingine mbali mbali.
Afisa elimu mkoa wa Njombe Mwalimu Nelasi Mulungu ametoa taarifa hiyo katika kikao cha ushauri ya mkoa (KUM) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe.
"Bado utoro upo,watoto 963 kwa mkoa mzima hawajafanya mtihani wa kidato cha pili,hawa walianza kidato cha kwanza vizuri lakini walipoingia kidato cha pili wakawa wamepotea kwasababu mbali mbali"amesema Nelasi Mulungu
Mulungu ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana Ili kudhibiti vitendo vya utoro kwa watoto kwa kuwa wanakosa haki yao ya kupata elimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...