Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, akizungumza na
mawakala waliojitokeza kwenye uzinduzi wa mafunzo ya bima kwa mawakala,
yanayotolewa na Benki ya NBC pamoja na Jubilee Alience Insurance kupitia
Chuo cha Bima na Hifadhi ya Taifa(ACSID). Jumatatu 21 Novemba,2022,
Posta-Dar-es-Salaam.
Benki ya Jubilee Allianz zafanya semina ya siku nne kwa mawakala wa NBC kuwapa elimu ya bidhaa mbalimbali za bima
Lengo ni kuunga mkono ajenda ya serikali ya huduma za kifedha jumuishi na kuweka huduma za kibenki karibu na wananchi.
Benki
ya NBC ina zaidi ya mawakala 8000 nchi nzima Dar- es – Salaam –
Novemba 22, 2022. Ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuimarisha utoaji wa
huduma za bima nchini, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeshirikiana
na Jubilee Allianz kutoa mafunzo kwa mawakala wa Benki hiyo (NBC Wakala)
na kuwapatia vitendea kazi na maarifa ya huduma za bima katika lengo la
kukuza mauzo. Mapema wiki hii, Benki kwa ushirikiano na washirika wa
bima ya Jubilee Alliance General Insurance, ilianza mafunzo ya wiki tano
kwa Wakala wa Benki hiyo ili kuwaelimisha na kuwapa taarifa za bidhaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, alisema benki hiyo
inaunga mkono ajenda ya Serikali ya huduma za kifedha jumuishi kwa
kuweka huduma za kibenki na bima karibu na wateja kupitia mtandao wa NBC
Wakala.
“Tanzania
ina kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma za bima katika Afrika
Mashariki, chini ya asilimia 1. Kwa mtandao mpana zaidi wa NBC Wakala
zaidi ya elfu nane kote nchini, tuna uhakika wa kuwafikia watu wengi na
kuwapa huduma hizi muhimu za bima. Tunatoa huduma mbalimbali za bima kwa
magari, mali, na ustawi kupitia bima ya maisha na afya,” alisema Sabi.
Sabi pia alieleza kuwa mawakala hao sasa watatumia mfumo maalum
uliotengenezwa na benki na washirika wake ili kurahisisha utoaji wa
huduma za bima. "Mauzo yetu ya bima kupitia mawakala yatafanywa kupitia
mfumo maalum uliotengenezwa na benki na washirika ili kufanya huduma
hiyo iwe ya kipekee, na ya kirafiki na jumuishi," alibainisha.
Kwa
upande wake, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA),
Dk. Baghayo Saqware, aliipongeza Benki ya NBC na Jubilee Allianz kwa
kutekeleza wito wa Serikali wa kupanua wigo wa huduma na bidhaa za bima
nchini. Dk Saqware alikumbusha kuwa Mei 2022, Mamlaka ya Usimamizi wa
Bima Tanzania (TIRA) kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango,
ilitoa mwongozo unaoelekeza makampuni na watoa huduma za bima kusajili
maafisa mauzo wa bidhaa za bima nchini.
“Nimefurahi
kuona kwamba Benki ya NBC imekuwa ya kwanza kuitikia azma hii, na kwa
kushuhudia mafunzo haya, hakuna shaka kwamba kutakuwa na upatikanaji
mzuri wa huduma ya bima nchini kote. Ninaipongeza NBC na Jubilee Allianz
kwa kuongoza katika mpango huu, na ninatumai kuwa taasisi nyingi zaidi
pia zitashiriki. Baada ya muda mfupi, Watanzania wengi watakuwa na
upatikanaji rahisi wa huduma za bima,” alisema Dk. Saqware. Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Jubilee Allianz, Bw.
Dipankar Acharya, alisema, “Hii ni fursa ya kusisimua kwa mawakala na
umma kupata bima ya afya kwa urahisi. Nimefurahishwa na ushiriki na
maswali yanayoulizwa. Hii inaonyesha tumejipanga katika kutoa huduma
bora za bima kote Tanzania.”
Mawakala
watafanya mafunzo na uhamasishaji wa kujiunga na bima zaidi kwa kufuata
michakato inayoratibiwa na TIRA na mamlaka nyinginezo ili kuhakikisha
kuwa huduma za haraka, zinazopatikana kwa urahisi na zinazofaa
zinatolewa. KAWAIDA [caption id="attachment_119859" align="aligncenter" width="2560"]
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...