Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Wawakilishi wa bara la Afrika katika Michuano ya Kombe la Dunia 2022, Senegal wameanza vibaya Michuano hiyo kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi katika mchezo wa Kundi A uliopigwa kwenye dimba la Kimataifa la Khalifa mjini Doha nchini Qatar.
Senegal walianza vizuri mchezo huo wa kwanza, wakiwashika vizuri Wapinzani wao, Uholanzi ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilienda sare ya bila kufungana (0-0).
Kipindi cha pili hadi dakika ya 80, Senegal waliendelea kuwashika ‘The Orange’ dakika ya 84 Uholanzi walipata bao la kwanza kupitia kwa Winga wa timu hiyo, ambaye anacheza Klabu ya PSV Eindhoven, Cody Gapko wakati bao la pili likifungwa na Kiungo wa Klabu ya Ajax, Davy Klaassen dakika ya 90+9.
Msimamo wa Kundi A baada ya michezo ya ufunguzi kwa timu hizo, Uholanzi wanaongoza Kundi hilo wakiwa na alama tatu, wakifuatiwa na Ecuador wenye alama kama hizo, Senegal wakiwa nafasi ya tatu bila alama yoyote kama walivyo wenyeji timu ya taifa ya Qatar.
Senegal wamepoteza mchezo wa kwanza wa Michuano hiyo, wanabaki Cameroon, Tunisia, Morocco na Ghana ambapo wanasubiriwa na bara la Afrika kutupa karata zao za ufunguzi wa Michuano hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...