Na John Walter-Manyara.


Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua mradi wa Vihenge nane mjini Babati wenye uwezo wa kuhifadhi tani 25,000 za mazao.

Akitoa taarifa hiyo afisa mtendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Milton Lupa amesema mradi huo uliojengwa kisasa umekamilika kwa asilimia 100 na vina uwezo wa kutunza chakula kwa muda wa zaidi ya miaka mitano bila kuharibika.

Amesema Rais Samia akiwa katika ziara mkoani Manyara Jumanne Novemba 22,2022 atazindua rasmi mradi huo uliogharimu Bilioni 19 na milioni 359 .Kukamilika kwa mradi huo ni fursa kwa ukanda wa Arusha,Kilimanjaro na Manyara kuhifadhi tani 70,000 za mazao ikiwa ni kiwango kikubwa kilichoongezeka ikilinganishwa na tani 39,ooo za uhifadhi wa hapo awali.

Aidha lupa ameongeza kuwa licha ya vihenge nane kujengwa lakini pia mradi umehusisha ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula yenye uwezo wa kuhifadhi tani 15 ikifanya idadi ya jumla ya uhifadhi wa vihenge na maghala kuwa tani 40,000.

Lupa ameeleza changamoto mbalimbali walizokutana nazo hadi kukamilika kwa mradi ikiwemo ugonjwa wa UVIKO 19 baada ya mkandarasi kushindwa kuendelea na mradi kutokana na hofu ya mkandarasi huyo kutoka nje ya nchi kuchangamana.Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Babati na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi hapo katika uzinduzi huo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...