MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani kijana Paul Meshack maarufu kama Kidevu (25), anayeishi Vingunguti jijjni Dar es Salaam baada ya kukiri kumuua bila kukusudia William Lupemba kwa kutumia mbao.
Kidevu ametiwa hatiani leo Novemba 23, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Suzan Kihawa.
Kabla ya kutiwa hatiani Wakili wa utetezi Rahel Salumbo aliiomba mahakama chini ya kifungu cha sheria cha 234 cha mwenendo wa makosa ya jinai kuondoa shtaka la mauaji ya kukusudia kuja kuwa mauaji ya bila kukusudia.
Upande wa mashtaka haukuwa na pingamizi na mshtakiwa akisomewa upya shtaka lake ambapo inadaiwa, Oktoba 4,2017 huko katika eneo la Vungunguti mshtakiwa Kidevu alimuua bila kukusudia William Lupemba.
Kabla ya kutiwa hatiani upande wa mashtaka ulimsomea mshtakiwa maelezo ya kosa ambapo ikaelezwa kuwa, siku ya tukio mshtakiwa Kidevu alikuwa eneo la Vungunguti lililopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Imeelezwa marehemu alikuwa amekana na dada aliyefahamika kwa jina moja la dada bonge ndipo alifika marehemu na kumwambia mshtakiwa kuwa anaonekana mchafu, maneno yaliyompa mshtakiwa hasira na kuanza kupigana.
"Katika ugomvi huo marehemu alichukua kisu na kujaribu kumchoma nacho mshtakiwa mara sita bila ya mafanikio ndipo mshtakiwa akachukua kipande cha mbao na kumpiganacho marehemu kichwani na mguuni ambapo alianguka na kufariki" ameeleza wakili Ester.
Imeelezwa kuwa mwili ulipelekwa Muhimbili kwa ajali ya kufanyiwa uchunguzi ambapo iligundulika kuwa marehemu alifariki baada fuvu la kichwa kupasuka kutokana na jeraha la kichwani.
Kufuatia hayo, mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa kituo kidogo cha polisi cha Pugu Mnadani na baadae alipelekwa kituo cha polisi Buguruni kwa mahojiano ndipo akafikishwa mahakamani.
Hata hivyo upande wa mashtaka alipoulizwa kama wanalolote la kusema dhidi ya mshtakiwa, wakili wa serikali Michael Shindai amesema hawana kumbukumbu za uhalifu wa mshtakiwa lakini pamoja na hayo wameiomba mahakama, itoe adhabu stahiki yenye kuleta fundisho kwa mshtakiwa na kwa jamii kwa ujumla.
"Hasa kwa kuzingatia, mshtakiwa ameondoa haki ya kuishi ya marehemu ambayo ni moja ya haki za msingi za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayolindwa na Katiba, mshtakiwa alijichukulia sheria mkononi kitendo ambacho hakipaswi kufanywa kisheria," alidai
Katika utetezi wake, wakili Sarumbo ameiomba mahakama impunguzie mshtakiwa adhabu.
"Mheshimiwa, mshtakiwa bado ni kijana mdogo wa miaka 25 tu aliyekuwa anafanya shughuli zake za kujipatia kipato na kujikimu na familia yake Vingunguti Dar es Salaam,"
"Mshitakiwa hakudhamiria kutenda kosa hili ila ni katika harakati za kutaka kuokoa uhai wake ikiwa ni baada ya kukwepa visu mara sita kutoka kwa marehemu na katika kujihami akajikuta ameua bila kukusudia," amesema Wakili Sarumbo.
Ameongeza kuwa mshtakiwa hana kumbukumbu ya makosa ya zamani, hili ni kosa lake la kwanza pia amekaa mahabusu kwa miaka mitano na amekuwa mtiifu kwa kipindi chote hicho na kwa kutambua kosa lake naiomba mahakama impunguzie adhabu na kama itaridhia apewe kifungo cha nje kwa kuwa hakudhamiria kutenda kosa hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...