Chifu wa Kabila la Wasangu wilayani Mbarali mkoani Mbeya Salehe Merere (Mwenye Kofia Nyekundu) akizungumza na waandishi habari waliotembelea Ikulu Chifu huyo Utengule kuhusiana na ukame wa maji kwenye bonde la Usangu/Ihefu.
Chifu wa Wasangu Salehe Merere akiwa na Baraza lake kwenye Ikulu ya Utengule wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mjumbe wa Baraza la Chifu wa Usangu anayewakilisha wanawake Kuluthum Merere akizungumzia kuhusiana wahamiaji katika bonde la Usangu wanavyoharibu mazingira na kusababisha ukame Ikulu ya Chifu Utengule wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Jengo la Chifu Merere likiwa katika hali kubomoka ambalo Chifu anaomba Wizara ya Maliasili na Utalii kuwasaidia jengo hilo.Chifu wa Wasangu Salehe Merere akiwa na Baraza lake kwenye Ikulu ya Utengule wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
*Ni wale waliovamia sehemu ya hifadhi ,laomba vijiji vya tambiko kuachwa
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV, Mbarali
BARAZA la Chifu la kabila la Wasangu limesema kuwa kukauka kwamto Ruaha kumechangiwa na shughuli za kibinadamu na kutaka Serikali kuchukua hatua kwa wavamizi kwenye bonde la Usangu.
Baraza hilo limetoa kauli wakati Kituo cha Wanahabari,Watetezi na Rasilimali na Taarifa (MECIRA) kilichofanya ziara katika Ikulu Chifu wa kabila la Wasangu juu ya uharibifu wa mazingira katika bonde la Usangu/Ihefu Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Akizungumza na waandishi habari katika Ikulu ya Wasangu Chifu Salehe Merere amesema kuwa hatua lazima zichukuliwe kwa Serikali katika kunusuru bonde la Usangu/Ihefu kutokana na kuendelea kufanyika shughuli za kibinadamu katika bonde hilo.
Amesema sehemu ya Ngiliama wananchi wamekuwa wakifanya kazi kama kawaida ikiwa na kwenda kuweka fedha za sarafu kwenye matambiko ya kabila la wasangu.
Chifu Merere amesema kuwa kuhusiana na tangazo la 28 'GN 28' juu ya mipaka ya hifadhi wanatambua lakini wanaomba kijiji cha Luhanga na Kalambo waachiwe kwa sababu ndio sehemu ya kufanyia matambiko.
Kwa upande wa Katibu Kabila la Wasangu wilaya ya Mbarali Simwasi Mutwa Magongo amesema kuwa viongizi wa vijiji wamekuwa wanaruhusu wenye mifugo kuwasajili kwenye vijiji vyao na mwisho wa siku wanaingiza katika hifadhi na kuharibu Ikolojia pamoja kukauka maji kutokana ng'ombe kushindilia mchanga na mwisho wa siku maji hayawezi kutiririka.
Amesema wakati mwingine wa viongozi wanaruhusu watu wenye makundi ya Ng'ombe kwa sababu ya rushwa.
Magongo amesema sehemu ya hifadhi iheshimike kwa wananchi kutofanya shughuli za kibinadamu kwani madhara yake ni makubwa kama yanavyoonekana kwa sasa.
Amesema kiongozi wa baraza la Chifu kwa wanawake Kuluthum Merere amesema kuwa wananchi wa usangu sio sehemu ya wamiliki wa shamba la Mnazi ambalo liko katika Hifadhi ya Ruaha.
Amesema kuwa hata vikao vyao juu ya sehemu Mnazi liko kwenye hifadhi wanafanyia mikoa mkoa mwingine ambapo watu wanaweza kuishi popotev ndani ya Tanzania lakini sio kuharibu mazingira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...