
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya Watanzania waliokuwa wakishiki kwenye Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi (COP27) mwaka huu uliofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh, nchini Misri, wakati alipotembelea Banda la Tanzania katika maonyesho ya mkutano huo. Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi nyingi duniani zilizohudhuria mkutano huo kwa udhamini wa Benki ya CRDB kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira. Mkutano huo ulijadili jitihada za namna ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo kuchapusha miradi ya kupunguza kaboni kwenye hewa. Mkutano huo ulianza Novemba 6 hadi 19, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazinngira, Suleiman Jaffo alipokuwa akizungumza, wakati alipotembelea Banda la Tanzania katika Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi
(COP27) mwaka huu uliofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh, nchini
Misri.
Maafisa wa benki ya CRDB wakiwa kwenye banda lao wakati wa Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi
(COP27) mwaka huu uliofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh, nchini
Misri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazinngira, Suleiman Jaffo (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa benki ya CRDB wakati alipotembelea kwenye banda lao katika Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi
(COP27) mwaka huu uliofanyika kwenye mji wa Sharm el-Sheikh, nchini
Misri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akikawa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania waliokuwa wakishiki kwenye Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa
mkataba wa Kimataifa wa tabianchi (COP27) mwaka huu uliofanyika kwenye
mji wa Sharm el-Sheikh, nchini Misri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...