Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MATOKEO ya utafiti uliofanywa na Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) John Costantino umeonesha mbinu mbalimbali za kilimo Ekolojia(kilimo Hai)zinazotumiwa na wakulima wadogo katika Wilaya ya Mvomero na Wilaya ya Masasi zimewafanya wakulima kuwa na uhakika wa kupata chakula cha kutosha.

Mwanafunzi huyo anafanya PHD na kwa sasa yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha utafiti wake ambao alioufanya kwa kuangalia uelewa wa matumizi ya kilimo ekolojia kwa wakulima wadogo katika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro na Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mratibu wa Taasisi ya Tabio Abdallah Mkindi amesema wameona iko haja ya kuwashirikisha waandishi wa habari kuhusu utafiti uliofanywa na mwanafunzi huyo wa SUA aliyeangalia mbinu kadhaa zinazotumika na wakulima wadogo katika kilimo ekolojia.Mbinu hizo ni kuchanganya mazao, kufunika ardhi, kupanda mazao yanayofunika udongo, kuchanganya kilimo, mazao ya kilimo pamoja na miti.

Pia mbinu nyingine ni kutumia samadi ya ng’ombe , mbolea vunde , kinyesi cha kuku, kinyesi cha nguruwe, matumizi ya mbolea inayotokana na kinyesi cha mbuzi na mbolea ya majani, kupanda mazao mbalimbali katika shamba moja au katika mashamba tofauti , kuchanganya kilimo na mifugo , matumizi ya dawa ya kudhibiti wa wadudu, dawa za kilimo hai, wakulima wanavyotumia mbegu za asili kurutubisha shamba ili kuruhusu rutuba iweze kurejea anapofanya kilimo mzunguko na pia jinsi ambavyo wakulima wanatumia mbinu mbalimbali za kukabiliana na mmomonyo wa udongo.

“Sasa katika hizi mbinu zinatumiwa na wakulima wa Mvomero na Masasi zimeonesha kuna muitikio mkubwa kwa hizi mbinu ambazo wakulima wanazitumia katika shughuli zao za kilimo na mwitikio huo unatuonesha katika eneo la kuchanganya mazao kwa Wilaya ya Masasi na wilaya ya Mvomero .Masasi ilikuwa karibu asilimia 94 ya wakulima wakuliokuwa wanachanganya mazao na zaidi ya asilimia 50 ya wakulima wa Mvomero walikuwa wanachanganya mazao.

“Na ukiangalia mfano wa mbegu za asili utafiti asilimia 78 kwa wakulima wa wilaya zote mbili walikuwa wanatumia mbinu za asili, kwa hiyo inaonesha kiasi gani cha mbegu ambacho wanatumia. Katika kuchanganya mfano mazao pamoja na mifugo zaidi ya asilimia 50 ya wakulima katika wilaya hizo wamechanganya kilimo na mifugo,”amesema Mkindi.

Amefafanua kwa hiyo hizo mbinu lengo lake kubwa ni katika kurutibisha udongo, kwasababu udongo ambao hauna rutuba hakuna mazao yanayoweza kuota , hivyo mbinu hizo utakuta zote kwa kiasi kikubwa zinalenga katika kurutibisha udongo na kuongeza unyevu ambao unamuwezesha mkulima kupata mafao yaliyo mengi.

“Kwa hiyo utafiti huu haukijikita katika kuangalia matokeo yatakuaje lakini umekuwa na muitikio mkubwa kwa wakulima na hata wakulima ambao hawakupata mafunzo wamekuwa na muitikio na Shirika la Swis Aid limekuwa likifanya kazi kubwa ya kuwajengea uwezo wakulima hasa kwenye kilimo ekolojia.Pia Shirika la Kilimo Endelevu(SAT) pia nao wanafanya kazi kubwa ya kuwajengea uwezo wakulima wa kutumia mbinu za kilimo ekelojia.

“Katika maeneo hayo wakulima wanafuga mifugo ya aina mbalimbali kama vile ng’ombe, mbuzi, kondoo, sungura , nguruwe ,kuku, bata , lengo ni kuwawezesha wakulima kupata chakula cha kutosha pamoja na uhakika wa kitoweo ambao usingewezekana kama wangekuwa wanafuga mfugjo mmoja.Pia kutokana na ufugaji huo wanapata mbolea ambayo wanaitumia kurutubisha mashamba.”

Aidha amesema kwa hiyo chakula kinachopatkana kinatumika kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kingine kuuza na katika wilaya hizo utafiti umeonesha hakuna mkulima anayelima zao moja bali wanalima aina mbalimbali za mazao kama vile mihogo, uwele , ufuta, mbaazi, kunde, choroko, karanga, na kwa Mkoa wa mtwara wanalima korosho , kakao, mpunga, maharage .

“Kwa hiyo wakulima wanapolima mazao haya mbalimbali kwanza wanakuwa na uhakika wa chakula karibia wakati wote kwasababu haya mazao mengine ni ya mizizi na unakuta hayavunwi kwa wakati mmoja, kwa hiyo mkulima anakuwa na uhakika wa chakula kwa ajili ya familia yake,

“Katika mazao hayo mengine yanakuwa kwa ajili ya biashara kwa mfano mazao jamii ya mafuta, karanga, alizeti hayo ni mazao ya kimkakati ambayo serikali imeweka nguvu , hivyo kumekuwa wa kupata kipato , kwa hiyo ukiangalia mazao kama mahindi Masasi na Mvemro zaidi ya asilimia 8o wamepanda hayo mazao.

“Utafiti huu unatupa matokeo kwamba umuhimu wa wakulima kuwa na mazao ya aina mbalimbali kwa ajili ya kuwa na uhakika wa chakula, cha ziada ili wauze kwa ajili ya kupata fedha na kujikimu kimazingira katika huduma nyingine katika maisha hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabianchi inatuonesha mbinu kama hizi zikitumika inawezesha kupata mavuno mengi na uhakika wa chakula,”amesema Abdallah.

Kwa upande wake Meneja Habari na Mawasiliano katika Shirika la Kilimo Endelevu (TOAM) Anatory Gabriel baada ya matokeo ya utafiti huo kazi kubwa ya waandishi wa habari pamoja na vyombo vyao ni kuhakikisha wanasaidia kufikisha tafiti na takwimu kwa wananchi kwa ujumla ili waone ni kwa namna gani kilimo ekolojia kinaweza kuifanya Tanzania kuwa na chakula wakati wote.

“Rai yangu mimi kama mtu ambaye nilishiriki katika utafiti huu kuweza kuona waandishi wanachukua hii mada kwa uzito wake na kutusaidia kuifikisha kwa watu wengi zaidi, unajua haya maandiko au machapisho na tafiti za kitaaluma zikiandikwa tu na kubaki kwenye makaratasi inakuwa vigumu kuwafikia watu wengi , hivyo kupitia waandishi itakuwa rahisi kufikisha kwa umma kwa kuandika kwa kutumia lugha rahisi inayoeleweka na kusomeka kwa urahaka,”amesema.

Ameongeza ni vema waandishi wakajifunza dhima kuu hasa ya kilimo ekolojia hasa ni nini ili waweze kufikisha ujumbe kwa wananchi ambao umekamilika.“Tukikaa tusubiri kupewa kila kitu itakuwa vigumu kuweza kuelewa na kufikisha ujumbe ambao umekusudiwa.hivyo machapisho tunayopewa tusome ili tufikishe ujumbe ambao umekusudia kuonesha namna gani kilimo ekolojia kinaweza kututoa katika hili baa la njaa ambalo linasababisha upungufu wa chakula na kufikia katika hali ya usalama wa chakula.


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...