Na Mwandishi Wetu

Timu ya taifa ya Ufaransa imejihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya mtoano ya 16 Bora ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Denmark katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Kundi D uliopigwa kwenye dimba la ‘Stadium 974’ nchini Qatar.

Ufaransa walijihakikishia nafasi hiyo kwa mabao yote mawili ya Mshambuliaji wa Klabu ya PSG, Kyllian MbappĂ© kwenye dakika ya 61’ na 86’ huku bao la Denmark likifungwa na Mlinzi wa timu hiyo, Andreas Christensen dakika ya 68’.

The Blues wameonyesha kiwango bora katika Kundi lao baada ya mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Kundi hilo kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Australia huku mzunguko wa pili wakipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Denmark.

Kikosi hicho cha Kocha, Didier Deschamps kinaongoza msimamo wa Kundi C kikiwa na alama sita, wakati Australia wakiwa kwenye nafasi ya pili wakiwa na alama tatu, nafasi ya tatu yupo Denmark mwenye alama moja pekee sawa na Wawakilishi wa bara la Afrika, Tunisia waliokuwa kwenye nafasi ya nne.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...