Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF) ulishiriki katika maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha
Kitaifa katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.
NSSF
ilitumia maonesho maonesho hayo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa
sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, matumizi ya mifumo ya TEHAMA kwa
mwanachama na mwajiri ili kumrahisishia huduma bila kulazimika kufika
katika ofisi za NSSF, kusikiliza na kutatua kero za wanachama na
kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo miradi ya nyumba za
kisasa, miradi ya uwekezaji ya majengo ya Mzizima Tower na Mwanza pamoja
na viwanja.Meneja
wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa akitoa elimu ya Hifadhi ya
Jamii kwa wanafunzi wa Chuo cha Utalii Mwanza waliofika katika banda la
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa Maonesho ya Wiki ya
Huduma ya Fedha jijini Mwanza.
Mkurugenzi
wa Hifadhi ya Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu, Festo Fute (wa pili kulia), Meneja wa NSSF Mkoa wa
Mwanza, Emmanuel Kahensa (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Hifadhi ya Jamii, Omary Mziya (wa kwanza kushoto) na Afisa Utawala Mkuu
wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Flora Ndutta (wa pili kushoto) wakiwa katika
picha ya pamoja baada ya viongozi hao kutembelea Banda la NSSF wakati wa
Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande, (kushoto) akipata
maelezo kutoka kwa Afisa Utawala Mkuu wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Flora
Ndutta (kulia), kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko katika
banda la NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini
Mwanza.Afisa
Utawala Mkuu wa NSSF Mkoa wa Mwanza Flora Ndutta (kushoto), akitoa
huduma kwa wananchi waliofika katika banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF) wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma ya Fedha jijini
Mwanza. (wa pili kushoto) ni, Mhasibu wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Said
Othman Mfuru.
Afisa
TEHAMA wa NSSF, Janeth Bwire, akitoa maelezo kwa mwanachama jinsi ya
kujihudumia kupitia simu yake kupitia mfumo wa WhatsApp chatbot. Huduma
hiyo inapatikana kwa njia ya Whatsapp ambapo mwanachama halazimiki
kufika Ofisi katika ofisi za NSSF. Elimu hiyo ya jinsi ya kutumia mifumo
inatolewa katika banda la NSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Huduma ya
Fedha jijini Mwanza.
Afisa
Matekelezo Mwandamizi, sekta isiyo rasmi Diagi Janguo akimwandikisha
Mwanachama mpya wa NSSF alipotembelea banda la NSSF kwenye Maonesho ya
Wiki ya Huduma ya Fedha jijini Mwanza
Afisa
Usalama Mwandamizi wa NSSF,Mfaume Kambangwa akitoa elimu kwa wanachama
wa NSSF waliotembelea banda la NSSF namna Mfuko unavyopinga vitendo vya
rushwa na kuwa huduma zote zinatolewa bure. Elimu hiyo ya kupinga rushwa
katika maeneo ya kazi inatolewa katika Maonesho ya Wiki ya Huduma ya
Fedha jijini Mwanza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...