Na mwandishi wetu,Ruvuma


Songea. Hemed Challe ameibuka Mshindi baada ya kumbwaga kwa kura 605 Aliyekuwa Mjumbe wa NEC mkoa wa Ruvuma Mussa Homera ambaye alikuwa akitetea nafasi yake bage ameambulia kura 52 kati ya 972 zilizopigwa na wajumbe.

Msimamizi wa Uchaguzi wa CCM Mkoa wa Ruvuma ,Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mataka amemtangaza Hemed Hamad Challe kuwa mshindi baada ya kupata kura 605

huku wapinzani wake Mussa Homera akipata kura 52 , Daniel Msembele akipata kura 258 na Edwin Millimga kura 30 ambapo wapiga kura ni 972 na kura zilizoharibika 27.

Kwa upande wake mjumbe wa Nec mkoa wa Ruvuma amewataka wanaccm kutulia na kuvunja makundi na kuwa na umoja kwani Uchaguzi limemalizika .

Hemed ameahidi wa CCM kuwa ataendelea kuwawakilisha kwa hekima na upendo.ili kuwaunganisha pamoja wakitumikie chama kuleta maendeleo kwa wananchi

Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo Wilbert Mahindi amesema mshindi alikuwa na anashahili kushinda kutokana na utendaji wake wa kazi uliotukuka pia amekuwa akiwaunganisha wanachama na kuwa wamoja huku akikemea matabaka ndani ya chama.

Cresensia Kapinga meibuka mshindi kwenye nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Mkoa kupitia CCM wilaya ya songea Mjini kwa kuwa mshindi wa kwanza kwa kupata kura 486 na kuwabwaga washindani wake wa karibu Luca Ngongi 401 , , Robert Mgowole 197,West Michael 273, Challe 160,Mapunda 43.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...