Na Mwandishi Wetu

Timu ya taifa ya Costa Rica imepoteza mchezo wake wa kwanza wa Kundi E la Michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar, baada ya kufungwa mabao 7-0 dhidi ya timu ya taifa ya Hispania kwenye dimba la Al Thumama.

Katika mchezo huo Hispania walianza kufungua akaunti ya mabao kupitia kwa Kiungo Mshambuliaji Daniel Olmo dakika ya 11', bao la pili lilifungwa na Marco Asensio dakika ya 21'.

Mabao mengiyyamefungwa na Mshambuliaji Fernando Torres 31' kwa mkwaju wa Penalti na dakika ya 54', linginge limefungwa na Pablo Gavi dakika ya 74', Carlos Soler dakika ya 90' na Alvaro Morata dakika ya 90+2'.

Licha ya kuwa na Wachezaji wao maarufu kama Golikipa Kaylor Navas, wengine Carlos Martinez na Yeltsin Tejeda, Costa Rica walishindwa kufurukuta mbele ya Uhispania waliokuwa na Nyota wake, Sergio Busquets, César Azpilicueta na wengine.

Kundi E la Michuano hiyo lina timu za Hispania, Japan, Ujerumani na Costa Rica.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...