Na Khadija Seif, Michuzi TV
WASANII wa Filamu Mkoa wa Dar es salaam waongoza kwa kazi zao kupitia kwenye mchujo wa awali katika Msimu wa pili wa tuzo za Filamu za kitanzania unaotarajiwa kufanyika Disemba 17,2022 Jijini Arusha
Akizungumza na Wanahabari Novemba 29,2022 Jiji Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo amesema kutokana na Makongamano pamoja na Semina mbalimbali ambayo yanafanyika kwa baadhi ya mikoa huku akiitaja Geita,Mbeya na Mkoa wa Dar es salaam imesaidia kwa kiasi kikubwa kukidhi kwa baadhi ya kazi kuingia kwenye mchakato wa awali wa kushindania tuzo za Filamu nchini.
"Tumebaini kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya mikoa kutopata elimu namna ya uandaaji wa kazi zao na namna gani zinaweza kuwa bora zaidi hivyo kwa mkoa wa Dar es salaam umeongoza kwa kazi 128 kuingia katika mchakato wa awali.
Hata hivyo Kiagho ameeleza kwa mwaka huu kumekuwa na mabadiliko na maboresha katika sehemu mbalimbali ikiwemo Kamati ya uratibu wa zoezi la kukusanya kazi iliweza kufika mikoa 25 ya Tanzania kukusanya kazi tofauti na mwaka jana 2021 kamati iliweza kuzunguka mikoa 7.
Aidha,Kiagho amefafanua zaidi Mkoa wa Dar es salaam ndio mkoa ulioongoza kwa kukusanya kazi 189 na filamu 127 zimeweza kukidhi vigezo huku Mkoa wa geita walikusanya kazi 9 na 4 kukidhi vigezo hivyo ikiwemo ubora wa picha, sauti, muongozo pamoja na mpangilio wa visa na matukio.
" Ni dhahiri kuwa makongamano yamekuwa na msaada tosha katika kuendeleza kuwapa msasa watayarishaji wa filamu na wasanii hususani kwa baadhi ya mikoa kupelekea kufanya vizuri kwa mchujo wa awali katika tuzo hizi ukiwemo mkoa wa Dar es salaam, Mbeya,Geita pamoja na Songwe."
Pia ameweka wazi mikakati ya bodi ya filamu kuhakikisha katika ukuaji wa sekta ya Sanaa itahakikisha watayarishaji na wasanii wanapewa semina mara kwa mara zitakazowajengea morali ya kufanya kazi zenye ushindani na zenye ubora wa Kimataifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu Emmanuel Ndumukwa amefafanua zaidi kuwa baada ya zoezi la mchujo wa awali wa filamu zilizofanikiwa kuingia kwenye mchakato kukamilika kinachofata ni nafasi ya kuzitazama filamu 151 ,ambapo ndani ya filamu hizo jopo la majaji litafanya kazi ya kuchagua zipi zitapigiwa kura na mashabiki.
Hata hivyo Ndumukwa ameongeza kuwa filamu 60% zitapigiwa kura na jopo la majaji huku 40% zitapigiwa kura na watazamaji ambapo zitaonyeshwa chaneli ya sinema zetu 103 kuanzia Novemba 30,2022 .
"Kazi zitaanza rasmi kuonyeshwa leo Novemba 29,2022 hadi Disemba 08,2022 sambamba na jopo la majaji litakaa na kuchagua filamu zitakazoingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo katika vipengele mbalimbali kuelekea kilele chake Disemba 17,2022 Jijini Arusha "
Kwa upande wake Msanii wa filamu na mtayarishaji kutoka Mkoa wa Mbeya Pius Nyange amesema Bodi ya filamu imeendelea kuamsha ari kwa wasanii kufanya kazi zenye ushindani kutokana na kuwepo wadau mbalimbali wanaounga mkono sekta ya Sanaa kwa ujumla.
Nyange pia ametoa pongezi kwa jopo la majaji kwa kukamilisha mchujo huo wa awali ambapo amefanikwa kupitia na kazi zake 3 ikiwemo Kosa,Kiganja,Karamu.
Hata hivyo wasanii waliopita kwenye mchujo huo ni pamoja na Lucas Mhuvile joti akifanikiwa kuingiza kazi 5 ikiwemo



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...