***********************************

Na Mwandishi wetu, Simanjiro

MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Dkt Suleiman Hassan Serera ameongoza harambee ya ujenzi wa ofisi za chama cha walimu Tanzania (CWT) Wilaya hiyo na kufanikisha kupatikana shilingi milioni 26.

Amesema fedha hizo zitafanikisha muendelezo mzuri wa ujenzi wa jengo hilo.

Hata hivyo, amewataka walimu kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwani Serikali imekamilisha madai yao mengi ya msingi.

Amesema walimu wa Simanjiro wamelipwa stahiki zao mbalimbali walizokuwa wanadai ikiwemo fedha za kujikimu, likizo, matibabu na posho nyingine.

“Walimu wamelipwa madai yao mengi hivyo serikali imetimiza wajibu wao ipasavyo nanyi timizeni wajibu wenu ili kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,” amesema Dkt Serera.

Katibu wa CWT Wilaya ya Simanjiro, Nazama Tarimo amemshukuru Dk Serera kwa kuongoza harambee ya ujenzi wa ofisi yao na kupatikana shilingi milioni 26.

Mwalimu Tarimo amesema chama hicho kipo kwa ajili ya kutetea na kuboresha maslahi ya walimu hivyo ofisi yao itasaidia wao kufanya kazi kwenye mazingira bora zaidi.

Amesema Wilaya hiyo ina walimu 929 wakiwemo maofisa elimu Kata 18 maofisa wa ofisi msingi na sekondari 10 TSC wawili wathibiti ubora wa shule watatu, walimu sekondari 277 na walimu wa msingi 617.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Simanjiro Kiria Laizer amesema walimu ni kada muhimu kwani ndiyo wanatengeneza wataalamu hivyo waungwe mkono.

“Kutokana na hali hiyo mimi binafsi nawachangia sh1 milioni ili mjenge ofisi yenu kwani mnasaidia kuwapa elimu jamii yetu,” amesema Laizer.

Diwani Kata ya Mirerani Salome Mnyawi amesema wataendelea kumuunga mkono mkuu huyo wa wilaya kwa namna anavyowahudumia wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...