ECOBANK Tanzania imetoa msaada wa vyereheni, khanga pamoja na Taulo za Kike katika Hospitali ya CCBRT iliyopo Msasani jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii katika maadhimisho ya uwajibikaji wa kijamii kwa kila mwaka ambayo huzishirikisha jamii zote ndani ya bara la Afrika. Nchi zote 33 Barani Africa zenye benki ya Ecobank zimekuwa zikitenga siku maalumu kila mwaka (Ecobank Day) kusaidia jamani zinazoizunguka ili kutumiza lengo la kurudisha kwa Jamii.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada wa  Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu alisema benki hiyo inautaratibu wa kila mwaka wa kurudisha kwa jamii ambapo leo wameamua kutoa msaada wa vyereheni, khanga pamoja na Taulo za Kike katika Hospitali ya CCBRT.

Amesema Ecobank Tanzania inadhamini mchango mkubwa wa hospitali ya CCBRT na ndio maana wameona walete msaada katika hospitali hiyo hasa kwa wasichana wanaojishugurisha na kushona ikiwa ni sehemu ya kuwainua watoto wa kike likiwa ni lengo kuu kwa mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi ameishukuru Ecobank Tanzania kwa kuweza kutoa msaada katika hospitali hiyo kwani kufanya hivyo inawapa nguvu ya kuendelea kutoa Huduma kwa jamii.

Amesema hospitali ya CCBRT itaendelea kutumia vifaa walivyopatiwa ili kuweza kuwainua watoto wa kike  kiuchumi nna kufika malengo waliyojiwekea 

Siku ya Ecobank ni tukio la kila mwaka ambalo kwa mara ya kwanza lilifanyika mwaka 2013, likiwa na mrengo wa kufanyika kila mwaka ikibeba kaulimbiu maalumu. Kaulimbiu hizi zimekuwa zikitoa Elimu kwa Vijana Wadogo Afrika (2013); Kuzuia na Kudhibiti Malaria (2014); kila mtoto wa Kiafrika ana haki ya kuwa na maisha bora ya baadaye (2015); Elimu ya TEHAMA shuleni na kuboeresha Afya ya Uzazi (2016); Usimamizi wa maji salama (2017); Makazi ya yatima (2018); Saratani (2019); Ugonjwa wa kisukari (2020) na Afya ya Akili(2021)  
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi Taulo za Kike ikiwa na lengo kurudisha kwa jamii ambapo Ecobank Tanzania imefanya hivyo katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi khanga ikiwa na lengo kurudisha kwa jamii ambapo Ecobank Tanzania imefanya hivyo katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, wafanyakazi wa Hospitali ya CCBRT pamoja na wadau mbalimbali kuhusu namna walivijipanga kila mwaka kurudisha kwa jamii mara baada ya Ecobank Tanzania kutoa msaada wa vyereheni, khanga pamoja na Taulo za Kike kwenye hafla iliyofanyika katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi akitoa neno la shukrani kwa Ecobank Tanzania kwa kuweza kuichagua Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kuwaomba Banki hiyo kuendelea kutoa misaada mbalimbali kwani bado changamoto kwenye hosptali hiyo bado zipo  mara baada ya kutoa msaada wa vyereheni, khanga pamoja na Taulo za Kike kwenye hafla iliyofanyika katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi mara baada ya kumalizika kwa makabidhiano ya vyereheni, khanga pamoja na Taulo za Kike kwenye hafla iliyofanyika katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada walioutoa kwa Hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi khanga pamoja na Taulo za Kike zilizotolewa na Ecobank Tanzania kwa Hospitali ya CCBRT ikiwa ni kurudisha kwa jamii wakati wamaadhimisho ya siku ya Ecobank Tanzania.
Baadhi Cherehani, khanga pamoja na Taulo za Kike zilizotolewa na Ecobank Tanzania kwa Hospitali ya CCBRT ikiwa ni kurudisha kwa jamii wakati wamaadhimisho ya siku ya Ecobank Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...