·    Wahasibu wanawake wapongezwa

Na Mwandishi Wetu

WAHASIBU na Wakaguzi wa Hezabu nchini wametakiwa kuweka mbele maslahi ya umma, kuwa waadilifu na kuzingatia maadili na sheria zinazowaongoza kwenye kazi zao za kila siku zza kihasibu.

 Wito huo ulitolewa Alhamisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali (NBAA), Profesa Sylivia Temu, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahasibu Duniani.

 “Tuzingatie uzalendo na maslahi ya taifa lakini pia nimewaasa tusijifungie kwasababu dunia imekuwa kama kijiji hivyo tujipange tuwe na mtazamo mpana ili tuweze kufanyakazi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa,” alisema

 “Nimewaambia wahasibu kwamba tumeshaandika hadithi ya miaka 50 iliyopita sasa tujiulize miaka 50 ijayo tunafanya nini ili tuwe endelevu tusiwe wale wale tu tunatakiwa kwenda sanjari na mabadiliko,” alisema

 Aidha, alisema bodi ya NBAA imeshaanza kuonyesha mfano kwa kufanya kazi za kihasibu kimataifa ambaapo wameanza kutoa ushauri nchini Msumbiji na Malawi na wanatarajia kwenda kwenye mataifa mengine.

 Alisema wahasibu na wakaguzi wanapopata kazi za kimataifa wasizikatae kwani zitailetea heshima nchi na  wahasibu wa Tanzania watapata sifa kwa umahiri na ubobezi kwenye fani hiyo na pia itawaongezea uchumi.

 Aliwataka wahasibu na wakaguzi wapambane kuikuza taaluma yao katika nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kwenda na kasi ya teknolojia duniani.

 “Tukiachwanyuma kiteknolojia nirahisi watu wengine wakafanyakazi ambazo siyo za uadilifu kwa kutumia teknolojia hiyo lakini sisi tukiwa vizuri kweneye teknolojia tutaweza kusimamia vizuri rasilimali fedha,” alisema

 Alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa mwenyekiti wa bodi wa kwanza mwanamke wa bodi hiyo kwa miaka 52 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972.

 “Namshukuru kwa kuniamini na muahidi kwamba nitafanya kazi na wenzangu kwa uaminifu mkubwa kuhakikisha fani hii inafanyika kwa uadilifu mkubwa,” alisema

 

Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno alisema maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka na sherehe hizo mwaka huu zinaenda sanjari na maadhimisho ya miaka 50 ya NBAA iliyoanzishwa 1972.

 Alisema NBAA imefanya mambo mengi kuongeza idadi ya wahasibu nchini ambao kwa sasa wako zaidi ya 26,000 na imefanya ukaguzi kwenye makampuni 450 kuangalia kama yanafuata matakwa ya sheria.

 “NBAA imeongeza idadi ya watahiniwa kwasasa mitihani  ambayo inafanyika Novemba au Mei kunakuwa na wanafunzi kama 7,000 wanaofanya mitihani hiyo na tumetoa miongozo mbalimbali,” alisema ,

 Alisema miongoni mwa mafanikio ya NBAA ni nchi mbalimbali kuja kujifunza namna ya kufanya kazi za kihasibu kwani kwa sasa NBAA inamkataba wa miaka mitano na serikali ya Msumbiji kufundisha masuala y uhasibu na fedha kwenye sekta ya umma.

 Alisema kwa miaka hiyo 50 NBAA imefanikisha kuwa na majengo yake yenyewe na akuwa na kituo cha Wahasibu Bunju APC na kwamba wamekutana kwenye maadbhimisho hayo wahasibu wa zamani na wa sasa kubadilishana mawazo namna ya kuboresha taaluma.

 “Kikubwa tumeambiana tufanye kazi kwa uadilifu na kwa kufuata taratibu miaka 50 ijayo tuendeleze matumizi ya TEHAMA na kwa sasa shughuli zote za NBAA zinafanyika kwa TEHAMA kasoro usimamizi wa mitihani pekee,” alisema CPA Maneno

 Alisema kutokana na kufanya vizuri kwenye sekta ya uhasibu Afrika imeitambua Tanzania kwamba inaongoza kwa usimamizi mzuri wa fedha kwenye sekta ya umma na ndiyo sababu ripoti ya Shirikisho la Wahasibu Duniani mwaka 2021 imeonyesha Tanzania na Nigeria ndizo zimefikia ubora wa viwango vya uhasibu vya kimataifa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali (NBAA), Profesa Sylivia Shayo, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahasibu Duniani iliyoandaliwa na Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA).
Mwenyekiti wa Chama cha wahasibu Wanawake Tanzania TAWCA, Dk. Neema Kiure akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahasibu Duniani iliyoandaliwa na Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA)
Baadhi ya wageni wakifuatilia mada mbalimbali kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahasibu Duniani yaliyofanyika Alhamisi Posta jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Chama cha Wanawake Wahasibu Tanzania (TAWCA)

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali (NBAA), Profesa Sylivia Shayo katikati akiwakaribisha wageni wengine kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahasibu Duniani iliyoandaliwa na Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno 

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali (NBAA), Profesa Sylivia, akiwaongoza wageni mbalimbali waliofika kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahasibu Duniani yaliyoandaliwa na Chama cha wahasibu Wanawake Tanzania TAWCA.

      

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...