Na.Veo Ignatus Arusha
Wakufunzi wa mpango wa Uwezeshaji kupitia Ujuzi (ESP) wametakiwa kuhakikisha wanabadilisha Maisha ya Wanawake katika kuondoka vikwazo vya ajira,kujiajiri na ujasiriamali,huku ikilenga kuimarisha uwezo wa washirika wake kwa kuwapa vyenzo na kusaidia kazi zao za kukuza usawa wa kijinsia , haki za binadamu,ushauri nasaha na ushauri wa kisaikolojia katika jamii.
Hayo yamesemwa na na Prof.Carolyne Nombo Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia katika mafunzo Jijini Arusha, katika utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto Tanzania, hasa kwa kuwawezesha wanawake kufuata fursa za kiuchumi na kijamii,pamoja na kuendeleza mazingira wezeshi kwa mahusiano ya usawa wa kijinsia
Prof.Nombo alisema kuwa Vyuo vya Maendeleo ya wananchi pamoja na AZAKI ni muhimu katika jamii kwani vinauweza wa kubadilisha maishabya wanawake na wanaume katika jamii kote Nchini Tanzania hasa kutokana na nafasi zao za kimkakati na dhana yao ya kuleta mabadiliko ya kijamii ndani ya nchi
Kwa upande wake Katibu wa kwanza Maendeleo ya ukuajiwa Uchumi wa ubalozi wa Canada Christopher Duguid alisema kuwa nchi hiyo inakivunia kuunga mkono ukuaji wa Mpango mpya wa mwitikio wa kijinsia nchini Tanzania,kupitia mpango wa uwekezaji kupitia ujuzi.
Aidha alisema mpango huo utatoa fursa kwa Canada kuendeleza uwekezaji wake mwingine,katika maeneo ya utekelezaji wa elimu usawa wa kijinsia ,haki za.kibinadamu ukuaji wa uchumi ambao unaofanya kazi kwa kila mtu
Dkt Alice Mumbi ni Mshauri wa Kiufundi wa ESP-Jinsia amesisitiza umuhimu wa kufikia malengo ya mwisho programu ambayo ni kuboreshwa kwa ushirika wa kiuchumi wa wanawake na wasichana vijana nchini Tanzania
"Iwapo jamii itahamasishwa na kuelimishwa juu ya umuhimu wa kutoa fursa sawa kwa wanawake na wanaume kutakuwa na mabadiliko chanya yatakayowawezesha kupata mafunzo na stadi za ujasiriamali kupitia FDCs na AZAKI.Alisema
Aidha mafunzo hayo, AZAKI washirika CDOs,FDCs na maafisa wa MoEST wataendelea kutoa mafunzo katika jumuiya na taasisi zao kwa wnaawake,wanaume na makundi mwengine wkaiwemo madereva bodaboda,daladala,viongozi w akimila ,kisiasa na kidini ,wazazi na watu wanaolengwa katika kuongeza uelewa na kutetea mabadiliko.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wakufunzi ToT yatakayowawezesha washiriki juu ya ukuaji wa uelewa wa jamii katika usalama wa Jinsia na Haki na Binadamu na kuitisha kikao cha Kamati ya Programu
Katibu wa kwanza Maendeleo ya ukuajiwa Uchumi wa ubalozi wa Canada ndugu Christopher Duguid:anajivunia uungwaji mkono wa ukuaji wa mpango mpya wa mwitikio wa Kijinsia Nchini Tanzania
Prof.Carolyne Nombo Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu sayansi na teknolojia,akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Place iliyopo Jijini Arusha yalipofanyika mafunzo kwaajiliya maelekezo mapana na mikakati ya inatolewa na PSC majukumu yake
Dkt Alice Mumbi ni mshauri wa Kiufundi wa ESP-Jinsia amesisitiza umuhimu wa kufikia malengo ya mwisho,na kusema anaamini jamii ikipatiwa elimu ya kutosha juu ya fursa sawa kwa wnawake na wanaume kutakuwa na mabadiliko chanya
Mnufaika wa Mafunzo hayo Mary Lenguije Laizer kutoka Taasisi ya Masai Stoves and Solar:mafunzo haya yamenisaidia kuelewa zaidi juu ya saikolojia ukatili wa kijinsia ambapo ameahidi kwenda kuwa balozi
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wakufunzi ToT yatakayowawezesha washiriki juu ya ukuaji wa uelewa wa jamii katika usalama wa Jinsia na Haki na Binadamu na kuitisha kikao cha Kamati ya Programu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...