Na Mwandishi Wetu

Timu ya taifa ya Ghana (The Black Stars) imefufua matumaini ya kufuzu hatua ya 16 Bora ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 baada ya kupata ushindi mabao 3-2 dhidi ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Korea Kusini kwenye mchezo wa Kundi H la Michuano hiyo.

The Black Stars wakiongozwa na Nyota wao André Ayew, Jordan Ayew, Inaki William na Thomas Partey wameonyesha kiwango bora na nidhamu nzuri ya ulinzi katika mtanange huo, mabao ya Ghana yalifungwa na Mohammed Salisu dakika ya 24’, na Mohammed Kudus aliyefunga mabao mawili dakika ya 34’ na 68’.

Wakiwa nyuma kwa mabao 2-0, Jamhuri ya Korea wakiwa na Nyota wao maarufu, ambaye anacheza katika Klabu ya Tottenham Hotspur, Son Heung-min walipata mabao yao ya haraka haraka kupitia kwa Cho Gue-sung katika dakika ya 58’ na 61’.

Kundi H la Michuano hiyo, Ureno wanaongoza wakiwa na alama tatu watakabiliana na Uruguay katika mchezo wa mzunguko wa pili, huku nafasi ya pili ni Ghana wenye alama tatu katika michezo miwili na Uruguay nafasi ya tatu na alama moja sawa na Korea walio kwenye nafasi ya nne.

Michezo ya mzunguko wa tatu, Ghana watacheza dhidi ya Uruguay, wakati Jamhuri ya Korea watapambana na Ureno ya Cristiano Ronaldo, michezo hiyo itaamua timu mbili zitakazofuzu hatua ya 16 Bora ya Michuano hiyo.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...