Na Mwandishi Wetu
Wawakilishi wa bara la Asia upande wa Mashariki, timu ya taifa ya Japan imepoteza mchezo wake wa mzunguko wa pili wa Kundi E dhidi ya timu ya taifa ya Costa Rica katika mchezo wa Michuano ya Kombe la Dunia uliopigwa kwenye uwanja wa Ahmed Bin Ali.
Bao la Costa Rica limefungwa na Mlinzi wa Kulia, Keysher Fuller dakika ya 81 ya mchezo. Japan walifanikiwa kupata ushindi katika mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Ujerumani wakipata ushindi wa mabao 2-0.
Costa Rica walifungwa mabao 7-0 na timu ya taifa ya Hispania katika mchezo wa kwanza wa Michuano hiyo.
Msimamo wa Kundi hilo, Hispania wanaongoza wakiwa na alama tatu wakiwa na mzunguko mmoja pekee wa Michuano hiyo, huku Japan, Costa Rica wote wakiwa na alama tatu katika mizunguko miwili huku Ujerumani akiwa hana alama yoyote ambapo atacheza na Hispania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...