Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Suleiman Mzee (kulia) akimsikiliza Meneja msaidizi wa uhusiano kwa umma kutoka Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Noves mosses (kushoto) alipokuwa akitoa maelezo juu ya shughuli mbalimbali za Benki hiyo wakati Mgeni huyo alipotembelea katika Banda la Taasisi hiyo leo Novemba 23,2022 kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Jijini Mwanza.

Maadhimisho hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya Rockcity Mall Jijini humo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Novemba 24,2022 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.

Meneja msaidizi wa uhusiano kwa umma kutoka Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Noves mosses (kushoto) akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Suleiman Mzee (kulia) alipokuwa akiuliza maswali kufahamu namna Benki hiyo inavyotekeleza majukumu yake.

Meneja msaidizi wa uhusiano kwa umma kutoka Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Noves mosses (kulia) akimkabidhi zawadi Mgeni huyo mara baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa meneja huyo.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Suleiman Mzee akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kumaliza ziara yake fupi kwenye Banda hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...