Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Cedric Kaze ameteuliwa na Uongozi wa Klabu hiyo kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu za vijana (U-17 na U-20) na timu ya Wanawake, Yanga Princess.

Taarifa ya Klabu hiyo, imeeleza kuwa Kocha Kaze ameteuliwa kushika nafasi hiyo huku akiendelea na majukumu yake ya Kocha Msaidizi wa timu kubwa ya Yanga SC.

Kaze akiwa katika majukumu yake ya ukocha kama Kocha Msaidizi wa timu hiyo, amepeta mafanikio msimu uliopita akiwa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi wakitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL), Kombe la Shirikisho (ASFC) na Ngao ya Jamii.

Hadi sasa, Kaze na Nabi wakiendelea kukinoa Kikosi cha Yanga SC hawajapoteza mchezo wowote wa Ligi za nyumbani wakiwa hawajafungwa michezo zaidi ya 40 (Unbeaten) tangu msimu uliopita wa 2021-2022





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...