Maswa Family Group ni kampuni ya kijamii yenye makao yake makuu mkoani Simiyu inayotatua changamoto ya uhaba wa chaki shuleni na taasisi za mafunzo nchini Tanzania.
Hoja ya Thamani inayoletwa na Maswa Group ni uwezo wake wa kuzalisha chaki zisizo na vumbi kwa wingi ambazo hukidhi mahitaji ya watu wengi nchini Tanzania na kupanuka kuelekea Kenya na uwezo wa kupunguza bei ya chaki.
Maswa Family Group imekuwa mnufaika wa mikopo ya Serikali ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kuweka msingi wa upanuzi wa biashara na kuanzisha mgodi wa jasi mjini Singida kama chanzo cha malighafi.
Kevin ameajiri zaidi ya wafanyakazi 30 kwa kazi rasmi na zisizo rasmi zilizopo mgodini Itigi na Simiyu, pia kutoa nafasi ya kupanua biashara kwa kuwa na maduka ya reja reja na mawakala katika miji mikubwa mbalimbali nchini.
KIJANA LEO ni Kipindi kinachoandaliwa na Jakaya Mrisho Kikwete Foundatio kwa Ushirikiano na Azam Media kupitia Chaneli ya UTV pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...