Na. Damian Kunambi, Njombe
Kijiji cha Nkwimbili kilichopo wilayani Ludewa mkoani Njombe ambacho hakijawahi kufikiwa na chombo chochote cha moto kinaenda kutengeneza historia mpya baada ya kuanza kutengenezwa kwa barabara inayoanzia katika kitingoji cha Iyinga mpaka Nkwimbili.
Barabara hiyo ambayo imetokana na ujenzi wa mnara wa simu unaojengwa na kampuni ya maqasiliano ya Tigo ambapo kupitia ujenzi huo wananchi hao wanaenda kupata faida mara mbili ambayo ni mawasiliano na barabara.
Alizungumzia hilo mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga mbele ya Naibu waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Kundo Methew amesema wananchi wa kijiji hichowamekuwa na kilio cha muda mrefu juu ya uwepo wa barabara hivyo amemshukuru Rais Samia Hassan kwa kuwapatia fedha za kuaezesha mawasiliano ambazo zimeenda kutatua changamoto mbili kwa wakati mmoja.
"Ndugu zangu ili kuweza kufikia eneo linalotakiwa kuweka mnara wa simu nilazima kuwepo kwa barabara nzuri itakayowawezesha kufikisha vifaa vya ujenzi kwa urahisi hivyo tayari mtambo wa kuchimba barabara hiyo umekwishaanza kazi hiyo"Amesema Kamonga.
Aidha katika upande wa mawasiliano ya simu naibu waziri Kundo amesema serikali imetoa fedha za ujenzi wa minara 6 yenye thamani ya zaidi ya Bl. 1.8 ambayo itakwenda kuwezesha upatikanaji wa mawasiliano kwa urahisi na kuondoa Changamoto hiyo kwa asilimia 100.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...